Mswada wa sheria kuhusu bangi nchini Uruguay unasikitisha: INCB

Kusikiliza /

INCB yaeleza wasiwasi kuhusu biashara ya bangi, Uruguay

Bodi ya Kimataifa ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya, INCB, imeelezea wasiwasi wake kuhusu mswada wa sheria ya kuruhusu uuzaji wa bangi kwa sababu zisizo za kimatibabu nchiniUruguay. Bodi hiyo imesema sheria kama hiyo itapitishwa, itakwenda kinyume na mikataba ya kimataifa kuhusu udhibiti wa madawa ya kulevya, hususan ule wa 1961, ambaoUruguaypia ilitia saini.

Bodi hiyo ya INCB  pia imeelezea masikitiko yake kufuatia serikali ya Uruguay kukataa kuupokea ujumbe wake kabla ya mswada huo kuwasilishwa bungeni. INCB imetoa wito kwa serikali yaUruguaykuhakikisha kuwa taifa hilo linaendelea kuheshimu sheria ya kimataifa ambayo inaruhusu matumizi ya dawa za kulevya, ikiwemo bangi, kwa minajili ya matibabu na utafiti wa kisayansi pekee.

Bodi hiyo imeongeza kuwa ikiwa mswada huo utapitishwa na kuwa sheria, huenda ukaathiri vibaya mno afya na maslahi ya raia, pamoja na kuzuia matumizi mabaya ya bangi miongoni mwa vijana.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Oktoba 2016
T N T K J M P
« sep    
 12
3456789
10111213141516
17181920212223
24252627282930
31