Mpanda milima afuturisha wasiojiweza na kutambua mchango wa WFP

Kusikiliza /

Amelie Zegmout

Akiwa amebobea kwenye shughuli za upandaji milima pamoja na shughuli za usamaria mwema, Bi Amelie Zegmout, amechukua fursa ya pekee kwa kuwakumbuka wale wasiojiweza kwenye mwezi huu mtukufu wa ramadhani kwa kuandaa futari na kuwafariji wale wasiojiweza.Amelie ambaye amekuwa akiishi Dubai kwa miaka 15 sasa anasema kuwa suala la usamaria mwema ni jambo linalopaswa kutekelezwa na kila mwenye uwezo na bila kuchagua sehemu ipi.

Kama njia mojawapo ya kutoa mchango wa kukabiliana na tatizo la njaa, katika siku za usoni amepanga kupanda mlima mrefu wa Mont Black kwa muda wa siku mbili.

Anatazamia kutimiza azma yake hiyo Agosti 11 na kwamba shughuli hiyo ya kupanda mlima ni sehemu ya kutambua mchango unaotolewa na shirika la mpango wa chakula duniani WFP, amnbalo lipo mstari wa mbele kukabiliana na tatizo la njaa.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031