Mjumbe maalum kuhusu masuala ya nyumba kufanya ziara uingereza

Kusikiliza /

Raquel Rolnik

Mjumbe maalum wa Umoja wa  Mataifa anayehusika na masuala ya nyumba Raquel Rolnik anatarajiwa kufanya ziara nchini Uingereza kuanzia tarehe 29 mwezi huu hadi tarehe 11 mwezi Septemba mwaka huu kutathimini sera na mipangilio iliyowekwa kutatua masuala nyumba, ubaguzi na mengine kuhusu haki ya kuwa na makao.

Rolnik anasema kuwa Uingereza imezungumzia kujitolea kwake katika kutimiza mambo yanayohusu haki za binadamu akiongeza kuwa ziara hiyo itampa fursa kutathimini suala hilo kwa kindani. Hii ndiyo ziara ya kwanza ya kukusanya habari inayofanywa na mtaaalmu huru aliyetwikwa jukumu na Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa kuchunguza na kuhakikisha kuwepo kwa haki ya kuwa na makao.

Akifanya ziara hiyo kwa mwaliko wa serikali mjumbe huyo maalum atazuru miji ya London, Edinburgh, Glasgow,Belfast na Manchester ambapo atakutana na maafisa wa serikali wanaohusika na masuala ya nyumba.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Aprili 2017
T N T K J M P
« mac    
 12
3456789
10111213141516
17181920212223
24252627282930