Mashirika ya misaada yaomba ufadhili zaidi kwa CAR

Kusikiliza /

Wakimbizi wa CAR

Mashirika ya kutoa misaada yametoa ombi la ufadhili zaidi ili kukidhi mahitaji ya kibinadamu katika Jamhuri ya Afrika ya Kati. Kati ya dola milioni 195 zinazohitajika kwa misaada ya kibinadamu, ni dola milioni 62 tu ndizo zilizopatikana, sawa na asilimia 32 ya fedha zinazohitajika.

Kwa mujibu wa Ofisi ya Kuratibu Misaada ya Kibinadamu katika Umoja wa Mataifa, OCHA, baadhi ya sekta kama maji na usafi zina uhaba wa ufadhili, ukiwa chini ya asilimia 8, huku zingine kama makazi na ukwamuaji wa mapema zikiwa hazina ufadhili wowote.

OCHA inasema uhaba huu wa ufadhili umelazimu mkwamo wa miradi muhimu ya kukarabati miundo mbinu na kuanza tena maendeleo ya kiuchumi. Aidha miradi inayowalenga watu walolazimika kuhama makwao na makazi ya dharura kwa wale wanaorejea haiwezi kutekelezwa.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Febuari 2016
T N T K J M P
« jan    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
29