Mashambulio Goma yasitishwe mara moja: Bi. Robinson

Bi. Mary Robinson

Mashambulio kwenye mji wa Goma, Mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC yanapaswa kusitishwa mara moja, ni kauli ya Mary Robinson, Mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwenye nchi za Maziwa makuu barani Afrika. Bi. Robinson amekaririwa katika taarifa iliyotolewa Jumamosi akisema kuwa mashambulio hayo yanasababisha madhila kwa raia ambao tayari wana kiwewe kilichosababishwa na miongo miwili ya mapigano, na hivyo hayakubaliki. Amesema kila jitihada zapaswa kuchukuliwa kuepuka mvutano zaidi kwenye eneo hilo, na badala yake ni vyema kuchagiza mashauriano na kuheshimu makubaliano ya amani, ulinzi na ushirikiano kwa ajili ya DRC na ukanda huo yaliyofikiwa mjini Addis Ababa mapema mwaka huu. Bi. Robinson amesema mapigano ya sasa yanatilia mkazo umuhimu wa haraka wa kupatia suluhu la kisiasa mzozo huo kwa mujibu wa maafikiano ya vikao vya hivi karibuni vya ukanda wa maziwa makuu. Mjumbe huyo maalum amezitaka mamlaka zote kwenye ukanda huo kujizuia kuhakikisha raia wanaoindwa na kupinguza uwezekano wa kundeleza mgogoro huo wakati huu ambapo anawasiliana na pande zote husika na kufuatilia hali ilivyo kwa karibu.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031