Mamlaka Misri lindeni mali za urithi wa kitamaduni: UNESCO

Kusikiliza /

Irina Bokova

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO Bi Irina Bokova ameeleza wasiwasi wake kuhusu maeneo ya urithi wa kitamaduni nchini Misri kufuatia ripoti za uporaji kwenye jumba la makumbusho la Kitaifa Malawi liliopo mji wa Minya na mashambulizi ya majengo kadhaa yalio na umuhimu wa kidini, yakiwemo makanisa na misikiti huko kaskazini mwa Misri, Fauyoum na Cairo.

Akilaani vitendo hivyo, Bi Bokova amesema vinaharibu historia na utambulisho wa raia wa Misri na ametoa wito kwa mamlaka za Misri kuhakikisha usalama na uadilifu wa majumba ya kitamaduni, maeneo na majengo ya kihistoria yakiwemo yale yalio na umuhimu wa kidini. Pia amezitaka kuzuia biashara haramu ya mali za kitamaduni zilioibwa kutoka jumba la makumbusho ya Kitaifa Malawi. Amesisitiza kuwa UNESCO iko tayari kutoa usaidizi wa kiteknolojia na kuhamasisha mashirika mengine yaliyoridhia mkataba wa 1970 dhidi ya biashara haramu ya urithi wa kitamadunii, yakiwemo INTERPOL na Idara ya Kimataifa ya Forodha.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031