Maisha ya wanawake na watoto huko Homs, Syria hatarini: UNICEF

Kusikiliza /

Mama na mwanae

Hali ya wanawake na watoto kwenye mji wa Homs nchini Syria inazorota kwa kasi ambapo raia Laki Nne kwenye wilaya ya Al Waer wamepoteza makazi yao na kulazimika kuishi kwenye mapagala, shule au majengo ya umma. Hiyo ni kauli ya Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto,UNICEFAnthonyLakealiyoitoa mjiniNew York, Marekani akieleza kuwa usalama huko Al Waer wazorota kila uchwao huku mashambulio ya makombora yakipamba moto na kusababisha majeruhi na vifo. Amesema UNICEF imekuwa ikisaidia washirika wake kusambaza misaada kama vile vyakula vyenye lishe pamoja na vifaa vya kujisafi bila kusahau majisafina salama kwa raia waliojikuta katikati ya mapigano. Hata hivyo amesema vituo vipya vya ukaguzi vinazuia upelekaji misaada zaidi kwenye eneohilohuku akitoa hadhari kuwa misaada ya dharurakamavile mboga za majani na maziwa vinapungua.Bwana Lake ametaka pande zote kuwezesha maeneo hayo kufikika salama ili familia ziweze kupatiwa misaada muhimu na wale wanaotaka kuondoka waweze kuondoka bila matatizo yoyote.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Mei 2017
T N T K J M P
« apr    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031