Maelfu wa wakimbizi wa Syria waingia Iraq:UNHCR

Kusikiliza /

Mkuu wa UNHCR Antonio Guterres

Mkuu wa Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR anasema kuwa maelfu ya wasyria walivuka mpaka na kuingia kaskazini mwa Iraq siku ya Alhamisi, kukitajwa kuwa kuhama kwa ghafla kunakowahusisha watu wengi. Jason Nyakundi na maelezo zaidi.

(Taarifa ya Jason)

Maafisa wa UNHCR walio nje wanasema kuwa watu wengi wanahama wakitumia daraja mpya iliyojengwa katika eneo la Pashakhabour. Kundi la kwanza la wasyria likiwa ni la watu 750 waliovuka daraja hiyo masaa ya mchana. Baadaye jioni kundi lingine la kati ya watu 5000 na 7000 lilifuatia. Adrian Edwards ni msemaji wa UNHCR.

(Sauti ya Adrian)

"Wengi wa wanaowasili sasa ni familia hususan kutoka Aleppo . Kiini cha kuhama huku kwa ghafla hakijulikani kwa UNHCR kwa sasa. Wasyria wengine wamekuwa wakisubiri karibu na mto Tigris kwa siku mbili au tatu."

Katika upande mwingine UNHCR inasema kuwa wiki hii imeanza kuwahamisha wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo waliovuka na kuingia mashariki wa Uganda tarehe 11 ,mwezi Julai kufuatia mashambulizi kutoka kwa kundi moja la waasi mashariki mwa DRC.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031