Madai ya matumizi ya silaha za kemikali Syria, Ban aagiza msaidizi wake aende Damascus

Kusikiliza /

Eduardo Del-Buey

Sakata la madai ya matumizi ya silaha za kemikali kwenye eneo moja huko Syria wiki hii limezidi kuchukua sura mpya baada ya Umoja wa Mataifa kujiandaa kuwasilisha ombi rasmi kwa serikali ya nchi hiyo iruhusu jopo lake kwenda eneo hilo kwa uchunguzi.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa Eduardo El Buey amewaambia waandishi wa habari mjini New York hii leo kuwa Katibu Mkuu Ban Ki-Moon ametaka uchunguzi ufanyike bila kuchelewa wakati huu ambapo tayari amemwagiza msaidizi wake kuhusu kuzuia kuenea kwa silaha Angela Kane aende Damascus, Syria.

(Sauti ya Eduardo)

"Tangu jana Katibu Mkuu amewasiliana na viongozi mbali mbali duniani kuhusu suala hilo. Na sasa anataka jopo la Umoja wa Matafa lililoko Damascua liruhusiwe haraka kuchunguza tukio hilo la asubuhi ya tarehe 21 Agosti mwaka 2013. Ombi rasmi linawasilishwa na Umoja wa Mataifa kwa serikali ya Syria kwa minajili hiyo. Bwana Ban anatarajia ombi kukubaliwa bila kuchelewa."

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031