Katibu Mkuu alaani ghasia zilizosababisha vifo nchini Misri

Kusikiliza /

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ambaye anahitimisha ziara yake Pakistani hii leo tayari kuelekea Jordan, amezungumzia ghasia zilizotokea mjini Cairo, Misri wakati vikosi vya usalama vikitawanya waandamanaji. Taarifa ya Joseph Msami inafafanua zaidi.

(TAARIFA YA JOSEPH)

Katika taarifa yake ya kulaani virugu hizo zilizotokea pale vikosi vya ulinzi vya Misri vilipotumia nguvu kuwaondoa waandamanji waliokuwa wamekusanyika , Katibu Mkuu Ban amesema wakati huu ambapo Umoja wa Mataifa unakusanya taarifa sahihi kuhusu tukio la leo amesikitishwa na mamalaka nchini humo kutumia nguvu katika kukabiliana na maandamano.

Bwana Ban amesema anatambua kwamba raia wengi wa Misri wamechoshwa na maandamano yanayovuruga utaratibu wa maisha yao ya kila siku na kwamba wanataka nchi yao ipate amani na mafanikio ya demokrasia hivyo akataka Wamisri wote kuelekeza nguvu katika kukuza upatanisho na umoja.

Amesema machafuko na uchochezi kamwe sio suluhisho la changamoto ambazo Misri inakabiliana nazo huku pia akisisitiza kwamba kupishana kwa mawazo kuelezwe kwa kuheshimiana na kwa amani.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930