Jopo la UM lasubiri kibali kutoka serikali ya Syria

Kusikiliza /

Profesa Ǻke Sellström, Mkuu wa jopo la UM la kuchunguza madai ya matumizi ya silaha za kemikali Syria

Jopo la Umoja wa Mataifa lililoundwa kuchunguza madai ya matumizi ya silaha za kemikali huko Syria litaenda nchini humo mapema iwezekanavyo pindi serikali itakaporidhia mpango kazi wake. Kauli hii ya hivi punde ni taarifa kutoka kwa msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwenda kwa waandishi wa habari ambapo amesema mwishoni mwa wiki iliyopita, mkuu wa jopo hilo Profesa Ake Sellström kutoka Sweden alikamilisha maandalizi yanayotakiwa kwa ajili ya ziara hiyo nchini Syria. Kinachosubiriwa hivi sasa  kwa mujibu wa taarifa hiyo ni kibali cha kuridhia kutoka serikali ya Syria. Wakati huo huo, Mkuu wa masuala ya kutokomeza silaha wa Umoja wa Mataifa Angela Kane ameendelea na mashauriano yake na serikali ya Syria kwa minajili ya kufikia makubaliano  haraka iwezekanavyo juu ya mpango kazi na hatimaye jopo la Umoja wa Mataifa liweze kufanya kazi yake kwa usahihi, usalama na lijitosheleze.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Febuari 2016
T N T K J M P
« jan    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
29