Hakuna sababu za kutosaini mkataba kupinga majaribio ya nyuklia

Kusikiliza /

Majaribio ya nyuklia

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema ingawa miaka 20 imepita tangu mkutano wa upokonyaji silaha uanze majadiliano ya mkataba wa kupinga majaribio ya nyuklia CTBT, mkataba huo bado haujaanza kutekelezwa.

Ban ameyasema hayo katika ujumbe maalumu wa maadhimisho ya nne ya siku ya kimataifa ya kupinga majaribio ya nyuklia ambayo kila mwaka huadhimishwa Agosti 29. Nchi 183 duniani zimetia saini mkataba huo huku zingine 159 zimeuridhia. Ban amesenma hatua imara naya mshikamano kuhusu majaribio ya nyuklia imedhihirika mapema mwaka huu baada ya watu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya watu wa Korea kuungana na jumuiya ya kimataifa katika kupinga majaribio ya nyuklia, hata hivyo Ban ameongeza kuwa mataifa mengine bado yamejizuia kuchukua hatua na hivyo kuzuia kuanza kutekelezwa kwa mkataba huo. Amesema hakuna sababu au mazingira ya msingi ya kuchelewesha zaidi lengo la utekelezaji wa mkataba huo.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Oktoba 2014
T N T K J M P
« sep    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728293031