FAO yaanisha umuhimu wa kukuza ushirikiano wa Kusini-Kusini

Kusikiliza /

Mawaziri wa kilimo kutoka Africa na Argentina

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la chakula na kilimo FAO  José Graziano da Silva amesema ni muhimu kuimarisha ushirikiano wa kanda ya Kusini-Kusini na yeye binafsi yuko tayari kupiga jeki uhusiano wa kibiashara baina ya Amerika ya Kusini na eneo la Kusin mwa Sahara kwa shabaha ya kukuza shughuli za kilimo. George Njogopa na taarifa zaidi.

(Taarifa ya George)

Kauli ya Graziano da Silva inakuja katika wakati mawaziri wa Kilimo wakikutana kwa mkutano wao wa pili huko Buenos Aires, mkutano ambao unazingatia maelewano ya pamoja baina ya ukanda wa Sahara Kusini na Amerika ya Kusin.

Mkutano huo mbao unatazamia kufukia tamati August 21 umebeba kauli mbiu isemayo " Ufanisi wa kilimo kwa maendeleo endelevu". Moja ya agenda kuu kwenye mkutano huo wa pili ni kushagihisha ushirikiano kwa nchi zinazoinukia kimaendeleo.

Akizungumza kwenye siku ya kwanza ya Mkutano huo, Mkurugenzi huyo wa FAO alisema nci za Amerika Kusini zinapaswa kuchukua jukumu la usoni kusaidia maendeleo ya Afrika.

Tangu kuanzishwa kwa mpango huo wa ushirikiano mnamo mwaka 1996, kumekuwa na mafanikio makubwa ya ushirikiano baina ya pande zote mbili. Hadi sasa makubaliano ya kiushirikiano yaliyosainiwa yanafikia zaidi ya 50.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930