Baraza la usalama lakutana kujadili hali ya usalama Mashariki ya Kati

Kusikiliza /

Oscar Fernandez-Taranco

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limekutana mjini New York, Marekani kujadili hali ya mashariki ya kati ikiwemo suala la Palestina ambapo pamoja mambo mengine limemulika hali ya wasiwasiMisri,LebanonnaSyria. Assumpta Massoi na taarifa zaidi.

(Taarifa ya Assumpta)

Ripoti hiyo ya Katibu Mkuu iliyowasilishwa na Bwana Taranco imegusia kwa mapana hali ya usalama Mashariki ya Kati kuanzia suala la ujenzi wa makazi mapya unaofanywa naIsraelkwenye maeneo ya Palestina ambapo Bwana Ban amesema sualahilolinaondoa kuaminiana kati ya pande mbili hizo wakati huu ambapo suala la mataifa mawili linaendelea kujadiliwa. KuhusuSyriaamesema hali inazidi kuzorota kila uchwao wakati mapigano yakiendelea, wananchi wakikimbiila nchi jirani na misaada ya kibinadamu ikishindwa kuwafikia walengwa kutokana na hali tete ya usalama.

(Sauti ya Taranco)

"Kuwafikia wale wenye mahitaji bado ni changamoto. Umoja wa Mataifa na wabia wetu  wa misaada ya binadamu tunategemea Baraza la Usalama kusaidia kuwezesha kuwafikia wenye mahitaji Syria na nchi jirani. Msimamo wa Katibu Mkuu haujabadilika: hakuna suluhisho la kijeshi kwenye mzozo huu. Matakwa ya kihalali ya wasyria ya uhuru na utu hayatanyamazishwa kwa mtutu."

Kuhusu Misri, Bwana Taranco alieleza kuwa Katibu Mkuu ameshatoa taarifa kuhusu  hali ilivyo na kwamba…

 

(Sauti ya Taranco)

 " Kile kinachoendelea nchini Misri na athari zake kikanda, kinaendelea kutia hofu kubwa na kinahitaji sisi kuzingatia."

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Machi 2017
T N T K J M P
« feb    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728293031