Ban, Mfalme wa Jordan wafanya mazungumzo ya pamoja

Kusikiliza /

Katibu Mkuu Ban Ki-moon na Mfalme Abdullah wa Jordan(picha ya faili)

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon leo amekutana na Mfalme Abdullah wa Jordan ambako wote wawili wamejadiliana juhudi zilizoanzishwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani John Kerry juu ya kurejesha upya mazungumzo ya upatanishi baina ya Israel na Palestina.

 

Ban alipongeza pia juhudi za Mfalme Abdullah pamoja na serikali yake kuhakikisha kwamba mazungumzo hayo ya upatanishi yanafufuka upya.

Kuhusu Syria, Ban alielezea kuridhishwa kwake na moyo wa ukarimu unaonyeshwa na wananchi wa Jordan kwa kuwahifadhi wakimbizi wa Syria ambao sasa wamefikia nusu milioni.

Ama kwa upande mwingine, viongozi wote wamejadiliana kuhusiana na hali ya mambo nchini Misri ambako kumekuwa na vitendo vya uvunjifu wa amani. Ban ametaka kuzingatiwa utashi wa kisiasa ili kuondoka kwenye mkwamo uliopo sasa.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Febuari 2016
T N T K J M P
« jan    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
29