Ban azungumza kwa simu na waziri Nabil Fahmy wa Misri

Kusikiliza /

Waandamanaji nchini Misri

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, amefanya mazungumzo kwa njia ya simu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri Nabil Fahmy kuhusu hali ya mpito nchini humo.

Katika mazungumzo hayo, Bwana Ban amesisitiza kwamba harakati za kisiasa jumuishi na za amani ndiyo njia pekee ya kuweka mustakhbali unaofaa kwa taifa hilo. Ametaka ghasia zikomeshwe na kutoa wito kwa mamlaka za mpito kuhakikisha haki za kimsingi za raia wote wa Misri zinalindwa, zikiwemo haki za kujieleza na kujumuika.

Katibu Mkuu amerejelea wito wake kwamba rais wa zamani Mohammed Morsy aachiwe huru, na kuwahimiza viongozi wa Misri kuzindua harakati za maridhiano za kuaminika. Amewakumbusha pia kuwa wana wajibu wa kuamua mustakhbali wa taifa la Misri.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Septemba 2016
T N T K J M P
« ago    
 1234
567891011
12131415161718
19202122232425
2627282930