Ban awasihi viongozi wa Israel kuendeleza mazungumzo ya amani

Kusikiliza /

Katibu Mkuu Ban Ki-Moon na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, ambaye yuko ziarani nchini Israel, amesema mazungumzo ya moja kwa moja ndiyo njia pakee ya kupata suluhu la kuaminika kwa mzozo kati ya Israel na Palestina. Alice Kairuki na taarifa kamili

(TAARIFA YA ALICE)

Bwana Ban amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa Israel, wakiwemo rais, Waziri Mkuu na Waziri wa Ulinzi, pamoja na kuzuru kaburi la Waziri Mkuu wa zamani, Yitzak Rabin.

Akikutana na Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, Bwana Ban amesema amefurahia kuanza tena mazungumzo ya amani kati ya Israel na Palestina, akiongeza kuwa ili harakati za amani zifanikiwe, mazungumzo hayo yanatakiwa yapewe umuhimu unaofaa.

"Nawaambia watu wa Israel kuwa harakati hizi zinatakiwa na ni lazima zilete usalama zaidi na matumaini ya ukanda wenye utulivu zaidi. Nipo hapa kuwasihi viongozi wote kuendelea kwenye barabara ya amani, na kusisitiza ahadi ya pamoja ya kushirikiana kuufanya mwaka 2013 mwaka wa maamuzi makubwa kwa amani ya Israel na Palestina, na kwa ukanda mzima."

Na akikutana na rais wa Israel, Shimon Perez, ujumbe wake umekuwa ule ule wa amani

"Rais nami tunakubaliana kuwa mazungumzo ya moja kwa moja bado ndiyo njia ya kuaminika katika kutafuta suluhu. Natoa wito kwa pande zote kuepuka na vitendo vinavyoweza kuyavuruga mazungumzo. Pande zote zinatakiwa ziendeleze mazingira yanayofaa kwa harakazi za amani kuendelea mbele."

Bwana Ban pia amezungumzia matukio yanayoendelea katika nchi jirani za Syria na Misri, akisema anayafuatilia kwa wasiwasi mkubwa.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Machi 2017
T N T K J M P
« feb    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728293031