Ban amteua Specioza Wandira-Kazibwe wa Uganda kuwa mwakilishi wake kuhusu HIV/UKIMWI Afrika

Kusikiliza /

 

Dr. Specioza Wandira-Kazibwe

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, amemteua Dr.Specioza Wandira-Kazibwe wa Uganda kuwa mwakilishi wake maalum kuhusu masuala ya HIV na Ukimwi barani Afrika.

Dkt. Kazibwe atamrithi Dkt. Asha-Rose Migiro wa Tanzania, ambaye Katibu Mkuu amemshukuru kwa huduma yake ya kusifika kwenye Umoja wa Mataifa na kujitolea kwake kama mjumbe thabiti wa juhudi za Katibu Mkuu za kutokomeza unyanyapaa na ubaguzi unaotokana na HIV kote duniani.          

Speciosa Wandira-Kasibwe, ambaye aliwahi kuwa makamu wa rais wa Uganda, hivi sasa ni mshauri mkuu wa rais wa Uganda kuhusu masuala ya idadi ya watu na afya, na mwenyekiti wa halmashauri ya kituo cha kusaidia katika mikopo na ujasiriamali. Ana shahada ya Doctorate katika sayansi kutoka chuo kikuu cha Harvard, Marekani.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Julai 2016
T N T K J M P
« jun    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031