Ban amteua Nickolay Mladenov wa Bulgaria kuwa Mwakilishi wake Maalum Iraq

Kusikiliza /

Ban amteua Nickolay Mladenov

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, leo ametangaza kuteuliwa kwa Bwana Nickolay Mladenov wa Bulgaria kama Mwakilishi wake Maalum kuhusu Iraq, na Mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kuisaidia Iraq, UNAMI.

 Bwana Mladenov ataichukua nafasi ya Bwana Martin Kobler wa Ujerumani, ambaye Katibu Mkuu amemshukuru kwa huduma yake yenye ukakamavu na uongozi mwema wa ujumbe wa UNAMI.

 Bwana Mladenov ana uzoefu mkubwakamamfanyakazi wa huduma za umma. Aliwahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje waBulgariakati ya Februari 2010 na Machi 2013, ambapo aliongoza mashauriano kati ya nchi yake na wadau kadhaa, likiwemo suala la Mashariki ya Kati. Alipata pia kuhudumu kama Waziri wa Ulinzi waBulgariatokea Julai 2009 hadi Januari 2010, nakamamwakilishi katika bunge la Jumuiya ya Ulaya, EU.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2017
T N T K J M P
« jul    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031