Ban amteua Iván Velásquez Gómez kamishna dhidi ya ukwepaji sheria Guatemala:

Kusikiliza /

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mastaifa Ban Ki-moon leo ametangaza uteuzi wa Iván Velásquez Gómez wa Colombia kuwa kamishina wa tume ya kimataifa dhidi ya ukwepaji sheria nchini Guatemala (CICIG), iliyoanzishwa chini ya makubaliano baiana ua Umoja wa Mataifa na serikali ya Guatemala na kuanza kazi 4 Septemba 2007. Bwana Velásquez anachukua nafasi ya kamishina anayemliza muda wake Francisco Dall'Anese wa Costa Rica, ambaye ametumikia tume ya CICIG kwa miaka mitatu. Ban ametumia fursa hii pia kumshukuru Dall'Anese kwa juhudi zake za kukabiliana na ukwepaji sheria na kuimarisha mfumo wa taasisi za sheria na haki nchini Guatemala. Bwana Velásquez anauzoefu mkubwa katika masuala ya sheria na alifanya kazi kama hakimu msaidizi wa mahakama kuu ya Colombia. Pia anauzoefu wa masuala ya upelelezi na uendesha mashitaka alioupata wakati akifanya kzi kwenye ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali ya Colombia.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031