Ban alaani mauaji ya mlinda amani wa MONUSCO toka Tanzania

Kusikiliza /

Walinda amani, MONUSCO

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon amelaani vikali mauaji ya mlinda amani wa Kitanzania na kujeruhi wengine huko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo siku ya Jumatano.

Mauji hayo ya mlinda amani wa mpango wa Umoja wa mataifa nchini Congo MONUSCO yametokea baada kundi la wapiganaji wa M23 kushambulia walinda amani hao waliokuwa wakitekeleza wajibu wao. Walinda amani hao wa MONUSCO walikuwa wakiwalinda raia kwa ushirikiano na jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo FARDC huko Goma.

Ban ametuma salamu za rambirambi kwa familia na serikali za Tanzania na Afrika ya Kusini wanakotoka walinda amani hao. Ameongeza kuwa Umoja wa Mataifa unaendelea kujidhatiti na msimamo wake wa kuchukua hatua muhimu kuwalinda raia wa Congo.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2017
T N T K J M P
« jul    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031