Ban akutana na mkuu wa kudhibiti matumizi ya silaha za kemikali

Kusikiliza /

Ban Ki-moon na Ahmet Üzümcü

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekutana mjini the Hague na Mkurugenzi Mkuu wa Jumuiya ya uzuajiaji matumizi ya silala za kemikali Ahmet Üzümcü.

Viongozi wote wamezitolea mwito pande zilizoko kwenye mzozo nchini Syria kutoa ushirikiano wa dhati kwa wachunguzi wa Umoja wa Mataifa ambao wameanzisha uchunguzi dhidi ya uwezekano wa kutumika kwa silaha za kemikali katika moja ya matukio ya hivi karibuni.

Wamesema kuwa  matumizi ya aina yoyote ya silaha za kemikali hayapaswi kurudiwa tena na wameelezea masikitiko yao kuhusiana na mashambulizi hayo ya Agosti 26 ambako mamia ya watu walipoteza maisha kutona na kile kinachoelezwa kuwa athari zilizotokana na silaha za sumu.

Kadhalika walipongeza kazi kubwa inayofanywa na jumuiya ya kupiga marafuku matumizi ya silaha za kemikali.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930