Ban ahitimisha ziara yake Pakistani aahidi ushirikiano

Kusikiliza /

Katibu Mkuu Ban Ki-Moon na Waziri wa Pakistani Nawaz Sharif

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ambaye amehitimisha ziara yake nchini Pakistani tayari kuelekea Jordan amekuwa na mazungumzo na waziri Mkuu Nawaz Sharif ambapo wamejadili masuala kadhaa ikiwemo mchango wa Pakistani katika ulinzi wa amani, malengo ya maendeleo ya milenia na hali ilivyo nchini Afghanistan. Baada ya mazungumzo hayo, Bwana Ban na Bwana Sharif walishiriki mkutano na waandishi wa habari ambapo Katibu Mkuu amesema Pakistani ni mbia muhimu na inatekeleza dhima kubwa katika maeneo yote ikiwemo amani na maendeleo na akatoa hakikisho.

(Sauti ya Ban)

"Nimemhakikishia Waziri Mkuu kuwa Umoja wa Mataifa utaendelea kusaidia Paksitani katika vita dhidi ya ugaidi na pia kuchochea kuvumiliana, na kuelewana miongoni mwa wananchi. Naunga mkono kwa dhati kabisa jitihada za kukabiliana na changamoto zinazokabili nchi yenu na wakati huo huo kuimarisha ujirani mwema. Tumejadili usaidizi wa Pakistani kwa kipindi cha mpito nchini Afhganistani mwaka 2014 pamoja na jukumu la Umoja wa Mataifa."

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031