Baraza la Usalama lapongeza kutekelezwa kwa mkataba kuhusu rasi ya Bakassi

Kusikiliza /

Baraza la Usalama

Wanachama wa Baraza la Usalama leo wamekaribisha kuhitimishwa kwa kipindi maalum cha mpito mnamo Agosti 13 2013, ambacho kiliwekwa kuhusu rasi ya Bakassi, chini ya makubaliano ya Greentree.

Baraza hilo la Usalama limezipongeza Cameroon na Nigeria kwa kutimiza ahadi zao na majukumu yao chini ya maamuzi yalofanywa na Mahakama ya Kimataifa ya Haki, na kwa kusuluhisha mizozano yao kuhusu rasi ya Bakassi kwa njia ya uwajibikaji na amani.

Baraza la Usalama pia limesifu juhudi za tume ya pamoja yaCameroonnaNigeriakatika kuwezesha utekelezaji wa majukumu yalowekwa na uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki, na katika kuweka mipaka ya ardhi na majini kati yaCameroonnaNigeria.

Wanachama wa Barazahilowamesifu mchango wa ofisi ya Umoja wa Mataifa Afrika Magharibi, UNOWA katika kuwezesha ufanisi huo, hususan Mwakilishi wa Katibu Mkuu kuhusu Afrika Magharibi kwa kusimamia tume ya pamoja ilowekwa kufuatilia utekelezaji wa makubaliano ya Greentree.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2017
T N T K J M P
« jul    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031