AMISOM yakashifu mashambuliz mjini Mogadishu

Kusikiliza /

Mjumbe maalum wa tume ya Muungano wa Afrika nchini Somalia (SRCC) balozi Mahamat Saleh Annadif amekashifu vikali misururu ya mashambulizi dhidi ya raia yaliyoshuhudiwa hiyo jana mjini Mogadishu nchini Somalia mashambulizi ambayo yanakisiwa kuendeshwa na kundi la Al-Shabaab. Watu kadha waliripotiwa kujeruhiwa kwenye mashambulizi hayo yaliyolenga kambi ya wakimbizi wa ndani na taa za barabarani zilizoezekwa na serikali kwenye barabara kuu ya mji wa Mogadishu.

Balozi Annadif anasema kuwa vitendo kama hivyo vya kundi la Al- Shabaab havina manufaa yoyote kwa watu wa Somalia bali ni vya uharibifu tu akiongeza kuwa kuwahakikishia usalama watu wa Somalia ndiyo ajenda kuu ya AMISOM. Mashabulizi hayo yanajiri wakati wasomali wanapojiandaa kusherehekea mwaka wa pili tangu wanajeshi wa Somalia na wale wa AMISOM kuwatimua Al- Shabaab kutoka mjini Mogadishu.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Oktoba 2017
T N T K J M P
« sep    
 1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
3031