Nyumbani » 28/08/2013 Entries posted on “Agosti 28th, 2013”

Ban akutana na kuzungumza na viongozi Uholanzi, amani duniani yaangaziwa.

Kusikiliza / Ban na viongozi Uholanzi

  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amekutana na kufanya mazungumzo na waziri mkuu na waziri wa mambo ya nje wa Uholanzi katika tukio la maadhimisho ya miaka mia moja tangu ujenzi wa kasri la amani lililoko The Hague Uholanzi. Katika mazungumzo yake na  waziri mkuu wa Uholanzi Mark Rutte , viongozi [...]

28/08/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Askari mmoja wa kulinda amani wa UM auawa Goma, watatu wajeruhiwa

Kusikiliza / Mlinda amanai auwawa , Goma

Umoja wa Mataifa umesema kuwa askari wake mmoja wa kulinda amani ameuawa na wengine watatu wamejeruhiwa wakati wa operesheni ya kijeshi huko Goma Kaskazini, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. Msemaji wa Umoja huo Farhan Haq amewaambia waandishi wa habari mjini New York kuwa operesheni hiyo ya kijeshi iliyoanza Jumatano asubuhi inaendeshwa na [...]

28/08/2013 | Jamii: Habari za wiki, Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Maendeleo au amani ya muda havina tija, viongozi sikilizeni wananchi wenu: Ban

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ametoa mhadhara kuhusu uhuru kwenye Chuo Kikuu cha Leiden huko The Hague, Uholanzi na kueleza bayana kuwa harakati zozote za kuweka amani au maendeleo ya muda hazina tija, kwani mambo hayo mawili yanapaswa kuwa endelevu. Ripoti ya Assumpta Massoi inafafanua zaidi. (Taarifa ya Assumpta) Majira ya asubuhi [...]

28/08/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kay akaribisha mkataba wa Juba uliosainiwa Addis Ababa:

Kusikiliza / Nicholas Kay

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia na mkuu wa UNSOM bwana Nicholas Kay leo amekaribisha mkataba uliotiwa saini mjini Addis Ababa kati ya waziri wa nchi Farah Sheikh Abdulkadir na Sheikh Ahmed Mohamed Islaan "Madobe"kwa niaba ya serikali ya mpito na utawala wa muda wa Jubba . Nayo Ethiopia ikiwa ni mwenyekiti wa [...]

28/08/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mtama waimarisha usalama wa chakula India.

Kusikiliza / Kilimo cha mtama India

  Kwa kipindi kirefu nchiniIndiamazao ya mchele na ngano yamekuwa yakipewa kipaumbele, hata hivyo wakulima hawajafanikiwa kupitia mazao hayo. Lakini sasa ziko habari njema kwa wakulima hususani ni wa zao la mtama ambalo huemda likanufaisha nchi na hata kusaidia katika usalama wa chakula.   Ungana na Grace Kaneiya kwa undani wa ripoti hii.

28/08/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Ban akutana na kuzungumza na waziri wa mambo ya nje wa Urusi.

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon akiwa ziarani nchini Uholanzi amekutana na waziri wa mambo ya nje wa Urusi Gennadiy Gatilov ambapo Bwana Ban amemueleza kiongozi huyo kuhusu kazi ya timu ya kuchunguza tuhuma za matumizi ya silaha za kemikali katika mgogoro unaoendeleaSyria. Pia viongozi hao wamejadili juhudi za kufanyika kwa mkutano [...]

28/08/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ban akutana na mkuu wa kudhibiti matumizi ya silaha za kemikali

Kusikiliza / Ban Ki-moon na Ahmet Üzümcü

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekutana mjini the Hague na Mkurugenzi Mkuu wa Jumuiya ya uzuajiaji matumizi ya silala za kemikali Ahmet Üzümcü. Viongozi wote wamezitolea mwito pande zilizoko kwenye mzozo nchini Syria kutoa ushirikiano wa dhati kwa wachunguzi wa Umoja wa Mataifa ambao wameanzisha uchunguzi dhidi ya uwezekano wa kutumika kwa [...]

28/08/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Hatua zimepigwa katika utendaji wa jeshi la polisi Haiti:UM

Kusikiliza / Sandra Honore

Mwakilishi wa mpango wa Umoja wa mataifa nchini Haiti MINUSTAH Sandra Honore amesema kazi kubwa iliyofanywa na MINUSTAH nchini Haiti inatokana na uwajibikaji na ujuzi wa jeshi la polisi la nchi hiyo na polisi wa Umoja wa Mataifa UNPOL. Kwa pamoja wakishirikiana na serikali ya Haiti wameweza kuweka mpango wa maendeleo wa mwaka 2012 hadi [...]

28/08/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Watu wengi wajitokeza kupiga kwenye kambi ya Dadaab:UNHCR

Kusikiliza / Wakimbizi katika kambi ya Dadaab nchini Kenya wapiga kura kuchagua mwakilishi wao

Kwenye kambi yenye ukumbwa wa mji mdogo uchaguzi wa aina yake kuandaliwa  unaelekea ukingoni. Zaidi ya theluthi moja ya wakimbizi 400,00 wnaoishi kwenye kambi ya Daadab nchini Kenya wamejindikisha kuwapigia kura wagombea 1,002 waanowania uongozi tofauti huku kila nafasi ikiwania na mgombea wa kiume na kike. Flora Nducha na taarifa kamili (RIPOTI YA FLORA NDUCHA) [...]

28/08/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Shambulio lolote dhidi ya Syria liidhinishwe na Baraza la Usalama: Brahimi

Kusikiliza / Lakdhar Brahimi

Shambulio lolote la kijeshi dhidi yaSyriani lazima lipate idhini kutoka baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, amesema Lakhdar Brahimi, mwakilishi wa pamoja wa Umoja huo na Umoja wa nchi za kiarabu nchiniSyria. Ripoti ya Jason Nyakundi yafafanua zaidi. (RIPOTI YA JASON NYAKUNDI) Akiongea mjini Geneva bwana Brahimi amesema kuwa anapinga hatua yoyote ya kijsehi [...]

28/08/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kasri ya amani The Hague yatimiza miaka 100, Ban azungumzia utawala wa sheria

Kusikiliza / Kasri ya amani, The Hague

Leo ni maadhimisho ya miaka mia moja tangu ujenzi wa kasri la amani lililoko The Hague Uholanzi, lenye ofisi za masuala ya sheria ikiwemo mahakama ya haki ya Umoja wa Mataifa. Sherehe hizo zimehudhuriwa na viongozi mbali mbali akiwemo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon aliyeelekeza hotuba yake zaidi kwenye masuala ya amani, [...]

28/08/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Watoto wengi Tanzania wako hatarini kutokana na kujihusisha na uchimbaji wa madini

Kusikiliza / HRW/Justin Purefoy

Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu Human Watch Jumatano limechapisha ripoti inayoelezea mazingira magumu wanayokumbana nayo watoto wanaojiingiza kwenye ajira ya uchimbaji madini nchini Tanzania, jambo ambalo linakiuka mikataba ya kimataifa ya haki za watoto ukiwemo wa shirika la kazi ILO unaopinga ajira ya watoto, na kueleza kwamba wengi wa watoto hao wanakabiliwa [...]

28/08/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kuheshimu haki za binadamu ni muhimu kwa utulivu DRC:Pansieri

Kusikiliza / Flavier Pansieri

  Vita dhidi ya ukwepaji sheria na kuheshimu haki za binadamu ni muhimu kwa kurejesha utulivu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo amesema naibu kamisha mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Flavia Pansieri , wakati akikamilisha ziara yake ya siku saba nchini humo. Alice Kariuki na taarifa kamili. (TAARIFA YA ALICE KARIUKI) [...]

28/08/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031