Nyumbani » 27/08/2013 Entries posted on “Agosti 27th, 2013”

Amani usalama, maendeleo vyamulikwa New York

Kusikiliza / Joseph Msami na Florence Makorere

  Warsha ya tatu ya muundo wa Umoja wa Mataifa inayohusisha wanafunzi wa vyuo mbalimbali duniani imeanza mjiniNew York, ambapo wanafunzi hao wamesema watayatumia mafunzo kama nyenzo  ya kukuza amani usalama na maendeleo.  Ungana na Joseph Msami aliyefanya mahojiano na wawakilishi wa Kenya na Tanzania katika warsha hiyo.               [...]

27/08/2013 | Jamii: Jiunge na Umoja wa Mataifa, Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Ban amteua Meja Jenerali Edy Mulyono mkuu wa kikosi cha MINURSO

Kusikiliza / minurso

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Kin Moon amemteua Meja Jenerali Edy Mulyono wa Indonesia kuwa kamanda mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa magharibi mwa Sahara (MINURSO). Taarifa iliyotolewa na msemaji wa Katibu Mkuu inasema Meja Jenerali Mulyono anachukua nafasi ya Meja Jeneral Abdul Hafiz wa Bangladesh, ambaye amekamilisha majukumu yake July [...]

27/08/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Feltman na viongozi wa Iran wajadili suala la Syria

Kusikiliza / Jeffrey Feltman

Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya siasa, Jeffrey Feltman amehitimisha ziara yake nchini Iran ambapo miongoni mwa mambo yaliyojitokeza wakati wa mazungumzo yake na viongozi waandamizi wa nchi hiyo ni hatma ya mgogoro wa Syria na nafasi ya Iran katika kupatia suluhu mzozo huo unaozidi kuathiri eneo la Mashariki ya [...]

27/08/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

IOM yaendesha mafunzo ya kukomesha usafirishaji wa binadamu Kusini mwa Amerika

Kusikiliza / IOM yatoa mafunzo kukomesha usafirishaji wa binadamu

Katika juhudi za kukomesha biashara haramu ya usafirishaji wa binadamu Amerika Kusini Shirika la kimataifa la Uhamiaji , IOM linaendesha mafunzo kwa askari, waendesha mashtaka na majaji  kutoka nchi tisa juu ya uchunguzi wa biashara hiyo. Mafunzo hayo ya siku nne yanafanyika mjini Buenos Aires, Argentina na yameandaliwa kwa ushirikiano kati ya IOM, mtandao wa [...]

27/08/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Bado kuna matumaini kufanyika mkutano wa pili kuhusu Syria: Brahimi

Kusikiliza / Watoto waliokumbwa katika mzozo nchini Syria

Mjumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa nchi za kiarabu nchiin Syria, Lakhdar Brahimi amesema hali nchini humo inazidi kuzorota kila uchwao na ni vyema pande zote zinazokinzana kufanya mazungumzo na kumaliza mgogoro huo kwa njia ya amani. Bwana Brahimi amesema hakuna upande wowote utakaoibuka na ushindi akiongeza kwamba kadri mzozo huo unavyoendelea,, [...]

27/08/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNAMA imelaani vikali muaji ya wafanyakzi raia:

Kusikiliza / Makao Makuu ya UNAMA

  Mpango wa Umoja wa Mataifa wa msaada Afghanistan UNAMA umelaani vikali vitendo vya karibuni vya utekaji na mauji ya raia sita kwenye jimbo la Herat. Miongoni mwa raia walionyongwa kulikuwepo wafanyakazi watato wa kamati ya kimataifa ya uokozi IRC shirika lisilo la kiserikali na mfanyakazi wa mpango wa kitaifa wa mshikamano. IRC ni mshirika [...]

27/08/2013 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Kutimuliwa Wapalestina Ukingo wa Magharibi kuwaitia hofu ofisi ya haki za binadamu:

Kusikiliza / human rights council

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imesema kitendo cha kuondolewa na kuhamishwa kwa nguvu kwa Wapalestina kwenye Ukingo wa Magharibi ikiwemo Jerusalem Mashariki kinawatoa hofu. Hatua hiyo imetokana na bomoabomoa inayoendeshwa na uongozi wa Israel katika maeneo sita tofauti kuanzia tarehe 19 Agost mwaka huu. Kwa mujibu wa taarifa ya ofisi ya [...]

27/08/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UNFPA yasema wanawake na wasichana wanapitia hali ngumu nchini Syria

Kusikiliza / Babatunde

 Mfuko wa idadi ya watu wa Umoja wa Mataifa UNFPA umeelezea wasiwasi wake kutokaka na athari ambazo zimesababishwa na ghasia ndani na nje mwa mji wa Damascus nchini Syria hususan kwa wanawake, vijana na familia zao. UNFPA pia imeshangazwa na kuongezeka kwa ghasia zinaowalenga raia sehemu zingine za nchi hali ambayo imewalazimu idadi kubwa ya [...]

27/08/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Misaada kwa wakimbizi kutoka Syria walio nchini Iraq yawasili Erbil

Kusikiliza / syria camp

Ndege ya kukodi ikiwa na vifaa vya misaada kutoka shirika la mpango wa chakula duniani, WFP na lile la wakimbizi, UNHCR imewasili hukoErbil,Iraq. Vifaa hivyo ni pamoja na mahema na biskuti zenye virutubisho na ni kwa ajili ya wakimbizi wa Syria waliokimbilia kaskazini mwa Iraq. Taarifa ya Grace Kaneiya inafafanua zaidi. (Ripoti ya Grace)  Zaidi [...]

27/08/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WHO yatoa mwongozo wa muda kutibu wagonjwa waliokumbwa na kemikali huko Syria

Kusikiliza / Nembo ya WHO

Shirika la afya duniani WHO hii leo limetangaza kuwa linatoa mwongozo wa muda wa tiba kwa wagonjwa waliokumbwa na kemikali nchini Syria. Mwongozo huo unazingatia mafunzo na maandalizi ambayo yamekuwa yakifanyika tangu mwaka 2012 kama anavyoripoti George Njogopa.  (RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA Mwongozo huo mpya unatajwa kuwa ni wa aina yake kutokana na kujumuisha taarifa [...]

27/08/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uchunguzi wa kemikali za silaha Syria waahirishwa kwa siku moja

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon na Ake Sellstrom anayeongoza timu inayochunguza madai ya m,atumizi ya kemikali, Syria

Kazi ya kuchunguza madai ya uwepo wa silaha za kemikali kwenye eneo moja karibu na mji mkuu wa Syria, Damascus, imeahirishwa kwa leo Jumanne baada ya uchunguzi kufanyika hapo jana. Assumpta Massoi na taarifa zaidi. (Taarifa ya Assumpta) Umoja wa Mataifa umesema jopo hilo likiongozwa na Profesa Ake Sellstrom lilikuwa liendelee na kazi hiyo Jumanne [...]

27/08/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNHCR yashutumu mauaji ya raia huko Mashariki mwa DRC,

Kusikiliza / Wakimbizi wa DRC

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limeungana na mashirika mengine  ya Umoja huo kushutumu mauaji ya raia mwishoni mwa wiki wakati wa mapigano kati ya jeshi la serikali na waasi wa kundi la M23 huko Goma, mji mkuu wa Jimbo la Kivu Kaskazini. Alice Kariuki na maelezo zaidi. (TAARIFA YA ALICE KARIUKI) [...]

27/08/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031