Nyumbani » 26/08/2013 Entries posted on “Agosti 26th, 2013”

Mjumbe maalum kuhusu masuala ya nyumba kufanya ziara uingereza

Kusikiliza / Raquel Rolnik

Mjumbe maalum wa Umoja wa  Mataifa anayehusika na masuala ya nyumba Raquel Rolnik anatarajiwa kufanya ziara nchini Uingereza kuanzia tarehe 29 mwezi huu hadi tarehe 11 mwezi Septemba mwaka huu kutathimini sera na mipangilio iliyowekwa kutatua masuala nyumba, ubaguzi na mengine kuhusu haki ya kuwa na makao. Rolnik anasema kuwa Uingereza imezungumzia kujitolea kwake katika [...]

26/08/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Wakaguzi wa UM watembelea hospitali huko Damascus

Kusikiliza / Msemaji wa Umoja wa Mataifa Farhan Haq

Hatimaye jopo la wakaguzi wa Umoja wa Mataifa limeweza kuendelea na kazi yake kwenye eneo linalodaiwa kuwa na silaha za kemikali kwenye viunga vya mji mkuu wa Syria, Damascus baada ya kushambuliwa na mshambuliaji wa kuvizia leo asubuhi. Msemaji wa Umoja wa Mataifa Farhan Haq amewaambia waandishi wa habari mjini New York, hii leo kuwa [...]

26/08/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

ILO yazindua nyenzo kupiga vita dhidi ya ajira ya watoto:

Kusikiliza / ILO yazindua muongozo katika harakati ya kukabiliana na ajira ya watoto

Shirika la kazi duniani ILO limezindua mafunzo ya muongozo wa hatua za kuongeza vita dhidi ya mifumo mibaya ya ajira ya watoto. Kwa mujibu wa ILO nyenzo hiyo mpya ina lenga kuchagiza juhudi za muongozo kuelekea lengo la kutokomeza mifumo mibaya ya ajira ya watoto ifikapo mwaka 2016.   Muongozo huo umeainisha maana ya mifumo [...]

26/08/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Wataalamu wa UM kukutana Geneva kujadilia mwongozo mpya wa haki za binadamu

Kusikiliza / Bendera ya Umoja wa Mataifa

Jopo la wataalamu wa Umoja wa Mataifa linalohusika na kukabiliana na mwenendo wa kuwatia watu kuzuizini kiholela, litakutana Geneva, Uswisi kwa ajili ya kuandaa mwongozo ambao utatumika kwenye vyombo vya mahakama wakati inaposikiliza kesi za kukabiliana na hali ya kukamata watu ovyo ovyo. Mmoja wa maafisa wa jopo hilo El Hadji Malick Sow amesema kuwa [...]

26/08/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Somalia bado kuna changamoto lakini hatukati tamaa: Kay

Kusikiliza / Nicholas Kay

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia, Nicholas Kay amehutubia baraza la amani na usalama la Umoja wa Afrika huko Addis Ababa,Ethiopia na kueleza kuwa takribani mwaka mmoja tangu kuundwa kwa serikali yaSomalia, bado changamoto ya usalama inakabili nchi hiyo.  Bwana Kay amesema eneo lenye utata zaidi ni Kusini mwaSomaliahususan mji [...]

26/08/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Kongamano linalomulika biashara na haki za binadamu kufanyika Colombia

Kusikiliza / Bendera za nchi wanachama, UM

Zaidi ya wajumbe 400 kutoka sekta mbalimbali duniani watakutana kwa kongamano la kwanza la Amerika Kusini na Caribbean lenye shabaha ya kujadilia namna biashara inavyoweza kuathiri haki za binadamu. Baadhi ya wajumbe kwenye kongamanohilo wanatazamiwa kutoa taasisi za kiserikali, mashirika ya kiraia, vyama vya kibiashara na wasomi wa kanda mbalimbali. Kongamano hilo ambalo ni kubwa [...]

26/08/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Maoni ya umma dhidi ya haki za binadamu DRPK yanasisimua: Kirby

Kusikiliza / Kiongozi wa jopo la UM kuhusu hali ya haki za binadamu, DPRK, Michael Kirby

Jopo la Umoja wa Mataifa lililoundwa kuchunguza hali ya haki za binadamu huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya watu wa Korera, DRPK kesho jumanne linaondoka Seoul Korea kusini kuelekea Tokyo baada ya kuhitimisha kazi ya kupokea maoni ya umma. Taarifa ya Grace Kaneiya inafafanua zaidi. (RIPOTI YA GRACE KANEIYA) Jopo hilo likiongozwa na Michael Kirby lipo [...]

26/08/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wakimbizi wa Somalia walioko Kenya huenda wakarejea makwao-UNHCR

Kusikiliza / Wakimbizi wa Somali walioko Kenya

Wakimbizi raia wa Somalia walioko nchini Kenya wanasubiri hatma ya majadiliano kati ya serikali ya nchi hiyo na Shirika la Umoja wa Matifa la  wakimbizi UNHCR nchini Kenya, ambapo serikali ya Kenya inadai usalama umeimarika Somalia kiasi cha kuwaruhusu wakimbizi hao kurejea nchini mwao. Hata hivyo zoezi hilo litatekelezwa kwa hiari. Emanuel Nyabera ni msemaji [...]

26/08/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mafuriko yaathiri maisha ya raia Sudan Kusini, misaada yahitajika.

Kusikiliza / Mafuriko, Sudan Kusini

Mafuriko yaliyotokea hivi karibuni nchini Sudan Kusini pamoja na mambo mengine yamesababisha athari za vifo, kukosa makazi na milipuko ya magonjwa. Janga hili limelazimu ujumbe wa Umoja wa Maataifa kufunga safari kuelekea humo kwa ajili ya kutoa misaada ya dharura. Ungana na Joseph Msami katika taarifa ifuatayo inayoangazia hali livyo nchini humo.  

26/08/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

UM wataka machafuko mapya DR Congo yakomeshwe:

Kusikiliza / Wahamiaji wanaokimbia mapigano, DRC

Huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo mwishoni mwa wiki kulizuka machafuko mapya kwenye eneo la Goma Mashariki mwa nchi hiyo na mwakilishi maalumu wa Umoja wa mataifa katika eneo la maziwa makuu Bi Mary Robinson kutoa kauli ya kutaka machafuko hayo yakomeshwe mara moja. Je hali ikoje kwa sasa? Mwandishi wa kujitolea Mseke Dide anaeleza [...]

26/08/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kamati ya UM kuhusu haki za watoto yasikitishwa na mauaji ya kutumia silaha za kemikali:

Kusikiliza / Mtoto, Syria, UNICEF

Kamati ya Umoja wa mataifa ya haki za watoto imesema madai ya shambulio la silaha za kemikali kwenye viunga vya Damascus Syria lililo katili maisha ya watu zaidi ya 300 wakiwemo watoto ni zahama na mfano wa kutisha wa jisni watoto wanavyolipa gharama ya vita nchiniSyria. Jason Nyakundi na maelezo kamili (TAARIFA YA JASON NYAKUNDI) [...]

26/08/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Msafara wa wachunguzi wa UM kuhusu matumizi ya silaha za kemikali washambukliwa

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon na Ake Sellström anayeongoza ujumbe wa uchunguzi, wa madai ya matumizi ya kemikali Syria

Syria, taarifa zinasema walenga shabaha wa kuvizia wameufyatulia risasi msafara wa wakaguzi wa Umoja wa Mataifa uliokuwa ukielekea kwenye eneo linaloshukiwa kuwa na silaha za kemikali. Assumpta Massoi na taarifa kamili (TAARIFA YA ASSUMPTA MASSOI) Gari ya kwanza ya wakaguzi hao wa silaha za kemikali lifyatuliwa risasi makusudi mara kadhaa na watu wasiojulikana katika eneo [...]

26/08/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930