Nyumbani » 21/08/2013 Entries posted on “Agosti 21st, 2013”

Ban awataka viongozi kuchukua hatua zaidi kufikia malengo ya kutokomeza umasikini:

Kusikiliza / KM Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amewataka viongozi wa dunia kuchukua hatua madhubuti ya kufikia malengo ya kutokomeza umasikini na mchakato endelevu. Ban ametoa ripoti muhimu kabla ya mkutano wa viongozi wa dunia utakaofanyika hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York tarehe 25 Septemba. Ripoti hiyo inatanabaisha nini kinachohitajika kufanyika kuchapuza [...]

21/08/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ni nuru njema kufuatia upatikanaji wa umeme wa nishati ya jua, Bangladesh

Kusikiliza / Nishati ya jua, Bangladesh

  Kufuatia miradi ya nishati ya jua sasa  maisha ya familia kadha Bangladesh yameimarika sio tu kwa kupunguza gharama aidha pia kupelekea watoto kufanya kazi zao za shule basi ungana na  Grace Kaneiya katika ripoti hii.

21/08/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Watu milioni 770 bado wanaupungufu wa vyanzo bora vya maji:UNDP

Kusikiliza / Upatikanaji wa maji safi na salama bado changamoto:UNDP

  Maji ndio kitovu cha machafuko ya kila siku yanayowakabili mamilioni ya watu duniani, yakitishia maisha, amani na usalama wa watu amesema afisa msaidizi wa shirika la Umoja wa Mataifa la maendeleo UNDP Rebecca Greenspan. Bi Greenspan ameyasema hayo kwenye mkutano wa kimataifa wa ngazi ya juu kuhusu ushirikiano wa maji unaoendelea huko Dushambe, Tajikistan [...]

21/08/2013 | Jamii: Habari za wiki, Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ban asikitishwa na tuhuma za matumizi ya kemikali leo Damascus

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amestushwa na tuhuma za matumizi ya silaha za kemikali leo  katika vitongoji mjini Damascus Syria. Katika taarifa yake aliyoitoa mjini New York Bwana Ban amesema atahakikisha uchunguzi wa kina wa tuhuma zilizowasilishwa katika ofisi yake. Tuhuma hizi zinakuja wakati huu ambapo timu ya Umoja wa Mataifa ya [...]

21/08/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM wapongeza miaka kumi ya mkataba wa amani Liberia:

Kusikiliza / Rais Ellen Johnson-Sirleaf

Maafisa wa ngazi za juu wa mpango wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani Liberia wamewapongeza watu na serikali ya Liberia kwa kudumisha amani kwa zaidi ya miaka kumi sasa na kuwataka washiriki ya kawaida wakizuia kurejea kwa machafuko kama siku za nyuma. Taarifa ya Alice Kariuki inafafanua zaidi: (TAARIFA TA ALICE KARIUKI) Katika taarifa [...]

21/08/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

IAEA kuzisaidia nchi za Sahel kusaka maji ya ardhini:

Kusikiliza / Isotope Hydrology Mauratania

Katika bara la Afrika eneo la Sahel ndio kame zaidi duniani na nchi zilizo katika eneo hilo zinakabiliwa na upungufu mkubwa wa maji huku watu wakitegemea maji ya ardhini na mahitaji ynaongezeka. Sasa shirika la kimataifa la nguvu za atomic IAEA linashirikiana na nchi za Sahel ili kubaini uwepo wa maji ardhini katika kanda hiyo [...]

21/08/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

IOM yaendeleza mafunzo kwa wakimbizi wa Rwanda

Kusikiliza / IOM-Logo

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM linaanza awamu ya tatu ya mafunzo ya wakimbizi wa Rwanda ambao walikimbia nchi hiyo kwa nyakati tofauti wakati wa machafuko. Mafunzo hayo ya stadi za kazi yanalenga kuwawezesha wakimbizi wanaorejea makwao kujikimu kimaisha kama anavyofafanua msemaji wa IOM Jumbe Omari Jumbe (SAUTI JUMBE)

21/08/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Bara la Afrika huenda likakabiliwa na ukosefu wa chakula ikiwa hatua hazitachukuliwa:UNEP

Kusikiliza / Food

Kutokana na kuwepo kwa mabadadiliko ya hali ya hewa kuna hofu kwamba bara la afrika huenda likakabiliwa na changamoto za ukosefu wa chakula ikiwa hatua madhubuti hazitachukuliwa. Inakadiriwa kuwa kati ta mataifa kumi yaliyo maskini zaidi duniani na yanayokabiliwa na tatizo la ukosefu wa chakula manane kati yao yako kwenye bara la Afrika. Jason Nyakundi [...]

21/08/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

FAO yaanisha umuhimu wa kukuza ushirikiano wa Kusini-Kusini

Kusikiliza / Mawaziri wa kilimo kutoka Africa na Argentina

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la chakula na kilimo FAO  José Graziano da Silva amesema ni muhimu kuimarisha ushirikiano wa kanda ya Kusini-Kusini na yeye binafsi yuko tayari kupiga jeki uhusiano wa kibiashara baina ya Amerika ya Kusini na eneo la Kusin mwa Sahara kwa shabaha ya kukuza shughuli za kilimo. George Njogopa na taarifa zaidi. [...]

21/08/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Umoja wa Mataifa umeazimia kupatia suluhu mzozo DRC: Kobler

Kusikiliza / Martin Kobler

Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC Martin Kobler amehitimisha ziara yake ya siku tatu huko Kivu Kaskazini na kusisitia azma ya Umoja huo katika kusaidia kurejesha mamlaka mashariki mwa nchi hiyo, amani na utulivu. Amegusia vikundi vyenye silaha huko Kivu Kaskazini na Kusini na maeneo mengine [...]

21/08/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930