Nyumbani » 20/08/2013 Entries posted on “Agosti 20th, 2013”

Wakimbizi wa Syria wamiminika Iraq

Kusikiliza / Wakimbizi wa Syria wahaha

Wakimbizi wa Syria walioko Iraq wanaendelea kuongezeka kila uchao. Wengi wao wakisema wanakimbia machafuko yanayoendelea kati ya vikundi vyenye silaha . UNHCR imesema Mmiminiko huu umepelekea upungufu wa Chakula, maji na umeme basi ungana na Joseph Msami katika ripoti hii  

20/08/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Mamlaka Misri lindeni mali za urithi wa kitamaduni: UNESCO

Kusikiliza / Irina Bokova

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO Bi Irina Bokova ameeleza wasiwasi wake kuhusu maeneo ya urithi wa kitamaduni nchini Misri kufuatia ripoti za uporaji kwenye jumba la makumbusho la Kitaifa Malawi liliopo mji wa Minya na mashambulizi ya majengo kadhaa yalio na umuhimu wa kidini, yakiwemo makanisa [...]

20/08/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

UNMISS yaimarisha doria jimboni Pibor

Kusikiliza / Wanajeshi wa kikosi cha UNMISS

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS, umeanzisha doria ya kijeshi katika jimbo la Pibor ili kuimarisha usalama katika eneo hilo na mji wa Gumuruk hatua itakayowezesha wananchi kurejea makwao na pia kuwezesha ugawaji wa misaada ya chakula. Kwa mujibu wa taarifa ya UNMISS, doria hiyo huendeshwa kila siku kwa kutumia magari na [...]

20/08/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Olimpiki 2016 Rio kujali mazingira na uendelevu: UNEP

Kusikiliza / UNEP_logo-298x300

Suala la uhifadhi wa mazingira na kuwa na dunia endelevu wakati wa michezo ya olimpiki ya mwaka 2016 itakayofanyika Rio de Janeiro nchini Brazili limepatiwa chepuo baada ya kamati ya maandalizi ya michezo hiyo na shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa kukubaliana mikakati mipya juu ya suala hilo. Chini ya makubaliano hayo UNEP itasaidia [...]

20/08/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

WFP yaingiwa hofu juu ya umaskini na ukosefu wa uhakika wa chakula Misri

Kusikiliza / WFP yatoa msaada wa chakula Misri

Shirika la mpango wa chakula duniani, WFP limesema lina hofu juu ya ongezeko la umaskini na ukosefu wa uhakika wa chakula nchini Misri hususan miongoni mwa jamii maskini wakati huu ambapo mzozo wa kisiasa unazidi kushamiri na hali ya uchumi ikidorora. Grace Kaneiya na taarifa kamili.  (Taarifa ya Grace Kaneiya) WFP imesema kuwa itaendelea kufuatilia [...]

20/08/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la usalama lakutana kujadili hali ya usalama Mashariki ya Kati

Kusikiliza / Oscar Fernandez-Taranco

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limekutana mjini New York, Marekani kujadili hali ya mashariki ya kati ikiwemo suala la Palestina ambapo pamoja mambo mengine limemulika hali ya wasiwasiMisri,LebanonnaSyria. Assumpta Massoi na taarifa zaidi. (Taarifa ya Assumpta) Ripoti hiyo ya Katibu Mkuu iliyowasilishwa na Bwana Taranco imegusia kwa mapana hali ya usalama Mashariki ya [...]

20/08/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

IOM yaisaidia Ufilipino kukabiliana na mafuriko

Kusikiliza / IOM yaitikia wito wa kuwasaidia wafilipino

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limeitikia ombi kutoka kwa serikali ya Ufilipino wakati mafuriko makubwa yanapoendelea kuwaathiri zaidi ya watu 600,000  kwenye mji mkuuManila. Tufani kwa jina Maring na upepo vimezua madhara kwenye nyanda za chini za mji wa Manila pamoja na sehemu zingine za milima kwa muda wa siku tatu zilizopita hali ambayo [...]

20/08/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkataba wa kimataifa kuhusu ajira za majini waanza kutumika rasmi leo: ILO/

Kusikiliza / Mkataba rasmim kuhusu ajira waanza kutumika Agosti 20:ILO

Mkataba wa kimataifa kuhusu ajira za wafanyakazi kwenye vyombo vya majini uliokuwa ukipigiwa chepuo na shirika la kazi duniani, ILO umeanza kutumika rasmi leo tarehe 20 Agosti 2013. Mkurugenzi Nkuu wa ILO Guy Rider amesema hizo ni habari njema na kwamba mkataba huo ni wa kihistoria kwani unalenga pamoja na mambo mengine kuhakikisha mazingira bora [...]

20/08/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Raia wengi wa Syria wanafurika Kaskazini mwa Iraq.UM

Kusikiliza / W2asyria wanokimbia kuelekea eneo la Kurdistan, Iraq

Idadi ya raia wa Syria wanaokimbia nchini mwao na kumiminika nchiniIraq inazidi kuongezeka kila uchwao ambapo tangu Alhamisi iliyopita, idadi yao imefikia Elfu Thelathini. Jana peke takribani wasyria Elfu Nne Mia Nane walivuka mpaka na kuingia Kaskazini mwaIraq. Ripoti ya Alice Kariuki inafafanua zaidi. (RIPOTI YA ALICE KARIUKI) Wengi wanaovuka mpaka huo ni wale wanaohofia [...]

20/08/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Watu 94,000 waathirika na mafuriko Ufilipino:OCHA

Kusikiliza / Mafuriko Ufilipino yaathiri watu 94,000:OCHA

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA imesema mvua kubwa za monsoon zilizoambatana na kimbunga Trami kinachojulikana nchini Ufilipino kama Maring imesababisha mafuriko na maporomoko ya udongo katika majimbo 11 na Manila mjini kwenye kisiwa cha Luzon. Serikali ya Ufilipino kwa mujibu wa OCHA inajikita hivi sasa katika kukabiliana mafuriko hayo [...]

20/08/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Tanzania kuanza kutimua wahamiaji wasio na vibali

Kusikiliza / Emmanuel Nchimbi

Serikali ya Tanzania leo imetangaza operesheni ya kuwatimua raia wa kigeni waliongia nchini humo kinyume cha sheria, ikiwemo wale waliorejea baada ya kuondoka nchini humo hivi karibuni, kutoka Dar Es salaam, George Njogopa anaarifu zaidi.  (Taarifa ya George) Bila kujata tarehe rasmi ya kuanza kwa operesheni hiyo, Waziri wa Mambo ya Ndani Emmanuel Nchimbi pia [...]

20/08/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ofisi ya haki za binadamu yasikitishwa na vifo na kushikiliwa watu Misri

Kusikiliza / Vurugu nchini Misri

Ofisi ya haki za binadamu inasikitishwa na idadi ya vifo vinavyoendelea kutokea Misri na pia kushikiliwa kwa viongozi na wafuasi wa kikundi cha Muslim Brotherhood. Kwa mujibu wa ofisi hiyo wale wote waliowekwa rumande haki zao lazima ziheshimiwe. Ofisi hiyo ya haki za binadamu inautaka uongozi nchini Misri kuruhusu kundi la waangalizi wa haki za binadamu [...]

20/08/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031