Nyumbani » 19/08/2013 Entries posted on “Agosti 19th, 2013”

Ban azungumzia wito wa SADC juu ya vikwazo dhidi ya Zimbabwe

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon

Hatma yoyote kuhusu vikwazo dhidi ya Zimbabwe ni kitu ambacho kinapaswa kujadiliwa na nchi wanachama au vyombo vya kikanda husika, ni kauli ya Katibu Mkuu Ban Ki-Moon aliyotoa leo mjiniNew York, Marekani wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari kuhusu ziara zake alizofanya Mashariki ya Kati na huko Pakistani. Kauli hiyo inafuatia swali la mwandishi [...]

19/08/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Shughuli za FIFA nchini Somalia zang’oa nanga

Kusikiliza / Kandanda , Somalia

Ni nuru njema kwa nchi ya Somalia kufuatia shughuli za Fifa na nchi hiyo kung'oa nanga kufuatia kuimarika kwa usalama na uthabiti wa nchi hiyo basi ungana na Joseph Msami katika ripoti hii

19/08/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Ulinzi wa raia kwenye mizozo bado ni changamoto, Ban ataka hatua zaidi

Kusikiliza / Baraza la Usalama

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limekuwa na mjadala wa wazi kuhusu ulinzi wa raia kwenye mizozo ambapo Katibu Mkuu Ban Ki-Moon amesema ulinzi wa raia unabakia kuwa moja ya mambo ya msingi kwa operesheni Tisa za ulinzi wa amani za umoja huo. Bwana Ban amesema hayo wakati wa mjadala wa wazi wa baraza [...]

19/08/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

UNESCO yalaani mauaji ya mwandishi nchini Libya

Kusikiliza /

Mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO Bi Irina Bokova amelaani mauji ya mtangazaji wa televisheni nchini Libya Azzedine Qusad yaliyotokea August 9 mwaka huu na kutaka uchunguzi ufanyike dhidi ya mauaji hayo. Katika taarifa yake Bi Bokova amezitaka mamlaka kuhakiisha waandishi wa habari wanafanya kazi katika mazingira [...]

19/08/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UM wakumbuka waliopoteza maisha wakisaidia wengine

Kusikiliza / Kumbukumbu ya watumishi, UM

Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya usaidizi wa kibinadamu Umoja wa Mataifa umefanya kumbukumbu ya watumishi wake waliopoteza maisha wakiokoa maisha ya wengine. Assumpta Massoi na taarifa zaidi. (Taarifa ya Assumpta) Kumbukumbu hiyo ya wafanyakazi 30 waliokufa kati ya Septemba mwaka jana na Juni mwaka huu imeandaliwa na Katibu Mkuu Ban Ki-Moon na imetilia [...]

19/08/2013 | Jamii: Habari za wiki, Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

CERF yatoa dola milioni 10 kwa misaada ya kibinadamu nchini Pakistan

Kusikiliza / Raia wa Pakistan wakipokea msaada wa chakula

Mfuko wa dharura wa Umoja wa Mataifa CERF umetenga kiasi cha dola milioni 10 kugharamia huduma za kibinadamu kwa zaidi ya watu milioni moja wasio na makao eneo la Khyber Pakhtunkhwa na sehemu za makabila nchini Pakistan kutokana na kuwepo ukosefu wa usalama tangu mwaka 2008. Jason Nyakundi na maelezo kamili. (RIPOTI YA JASON NYAKUNDI) [...]

19/08/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Naibu Kamishna wa haki za binadamu wa UM kuzuru DRC

Kusikiliza / Flavia Pansieri

Naibu Kamishna wa Tume ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa Flavia Pansieri baadaye wiki hii ataanza ziara ya wiki moja huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kama anavyo ripoti Grace Kaneiya.  (RIPOTI YA GRACE KANEIYA) Wakati wa ziara yake Pansieri atakutana na maafisa wa serikali ya DRC wakiwemo wale wa ngazi za juu [...]

19/08/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Maisha ya wafanyakazi wa misaada yaendelea kuwa hatarini: WFP

Kusikiliza / Wafanyakazi wa WFP

Shirika la mpango wa chakula la Umoja wa Mataifa WFP limetumia siku ya leo kukumbuka watu 22 waliopoteza maisha baada ya ofisi za umoja wa mataifa kushambuliwa hukoBaghdad,Iraq, ambapo WFP yasema miaka kumi baada ya tukiohilobado wafanyakazi wa misaada wanaendelea kuuawa wakitekeleza jukumu la kuokoa maisha yaw engine. George Njogopa na taarifa kamili. (TAARIFA YA [...]

19/08/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

ILO yapongeza kuanza kwa mkataba mpya unaohusu usafiri wa majini

Kusikiliza / ILO yakaribisha mkataba unaohusu usafiri wa majini

Shirika la kazi duniani ILO, limesema kuwa wakati mkataba wa wanamaji wa mwaka 2006, ukitarajia kuanza kufanya kazi August 20, nuru mpya wa matumaini inafunguka kwa watumishi wanaotumia muda wao mwingi wakiwa kwenye vyombo vya baharini.   ILO inasema kuwa kuanza kazi kwa mkataba huo kunamaanisha kuwa, sasa maelfu ya wafanyakazi watakuwa wakiendesha majukumu yao [...]

19/08/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Dunia yahitaji misaada zaidi ya kibinadamu: OCHA

Kusikiliza / Siku ya utoaji wa misaada ya kibinadamu

Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya utoaji wa misaada ya kibinadamu, Umoja wa Mataifa na wabia wake zikiwemo kampuni, wamechochea kampeni ijulikanayo dunia yahitaji zaidi ikiwa na lengo la kuhamasisha usaidizi wa watu waliokumbwa na majanga ya kibinadamu. Ofisi ya Umoja wa kimataifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu, OCHA imesema ni dhahiri ya kwamba [...]

19/08/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Maelfu ya Wasyria wavuka mpaka na kuingia Iraq:UNHCR

Kusikiliza / Wasyria wanaokimbia ghasia

Shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR linasema karibu Wasyria 20,000 wamevuka mpaka na kuingia Kaskazini mwa Iraq. Wakimbizi wengi wanasema wanakimbia mapigano yanayohusisha makundi yenye silaha na ongezeko la mvutano katika maeneo ya Kaskazini mwa Syria ikiwemo Efrin,Aleppo, Hassake na Qamishly. UNHCR inagawa maji na chakula kwa wakimbizi hao wapya wanaowasili, na [...]

19/08/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930