Nyumbani » 16/08/2013 Entries posted on “Agosti 16th, 2013”

Heko uchaguzi Mali, kilichobakia kuimarisha taasisi na utulivu: Wajumbe Baraza la usalama

Kusikiliza / Rais wa Baraza la Usalama Balozi Maria Cristina Perceval wa Argentina

Wajumbe wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa wamezingatia matokeo ya awamu ya pili ya uchaguzi nchini Mali kama yalivyotangazwa na mamlaka za mpito nchini humo ambapo Ibrahim Boubacar Keïta ametangazwa mshindi wa Urais wa nchi hiyo. Kwa mantiki hiyo wajumbe hao wamesifu wananchi wa Mali kwa jinsi walivyoshiriki kwenye mchakato wa uchaguzi kwa [...]

16/08/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Changamoto ya kukosa ajira iliibua fursa ya kujiajiri jijini Nairobi:

Kusikiliza / Vijana wakisomba takataka

Wiki mbili za mwanzo wa mwezi huu wa Agosti, kumefanyika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vijana, na kwingineko madhimisho hayo yanaendelea kwa ngazi ya kitaifa. Kubwa lililokuwa linamulikwa ni jinsi vijana wanahaha kuhama vijiji, mikoa na hata nchi zao kusaka ajira bora ali mradi mkono uende kinywani. Umoja wa Mataifa unasema kuwa hali ngumu [...]

16/08/2013 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Vitendo vya ukatili wa kingono na kijinsia vyashamiri Somalia: UM

Kusikiliza / Shida ya maji chanzo cha ukatili wa kingono Somalia

  Ofisi ya kuratibu misaada ya kibinadamu katika Umoja wa Mataifa OCHA imesema matukio ya unyanyasaji wa kijinsia na kingono nchini Somalia umeshamiri na kwamba katika kipindi cha miezi sita ya kwanza ya mwaka huu kumekuwepo na visa 800 vya aina hiyo kwenye mji mkuuMogadishu. George Njogopa na maelezo zaidi(Taarifa ya George) OCHA inasema kuwa [...]

16/08/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ukata wakwamisha miradi ya usaidizi wa kibinadamu Korea Kaskazini: OCHA

Kusikiliza / Watoto wakipata mlo wa msaada nchini Korea Kaskazini

Umoja wa Mataifa umesema kuwa miradi mingi inayotekelezwa na taasisi zake tano huko Korea ya Kaskazini, DPRK,  bado haijapata ufadhili wa kutosha. Umesema kuna hitajio la dharura za dola za Marekani milioni 90 ambazo ni kati ya dola milioni 150 zilihitajika kwa ajili ya mwaka 2013. Kiasi hicho cha fedha kinachohitajika kwa haraka ni kwa [...]

16/08/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ban awasihi viongozi wa Israel kuendeleza mazungumzo ya amani

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-Moon na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, ambaye yuko ziarani nchini Israel, amesema mazungumzo ya moja kwa moja ndiyo njia pakee ya kupata suluhu la kuaminika kwa mzozo kati ya Israel na Palestina. Alice Kairuki na taarifa kamili (TAARIFA YA ALICE) Bwana Ban amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa Israel, wakiwemo rais, Waziri [...]

16/08/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wataalamu wa haki za binadamu wataka kusitishwa kwa ghasia nchini Misri

Kusikiliza / Egypt demonstrations

Kundi la wataalamu wa masuala ya haki za binadamu kutoka Umoja wa Mataifa wametaka kusitishwa mara moja kwa ghasia ambazo zimesababisha vifo vingi pamoja na majejeraha mjini Cairo nchini Misri siku za hivi majuzi. Wataalamu hao wameshutumu kile ambacho wamekitaja kuwa matumizi ya nguvu kupita kiasi kutoka kwa vikosi vyta usalama wakisema kuwa maandano ya [...]

16/08/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Maelfu wa wakimbizi wa Syria waingia Iraq:UNHCR

Kusikiliza / Mkuu wa UNHCR Antonio Guterres

Mkuu wa Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR anasema kuwa maelfu ya wasyria walivuka mpaka na kuingia kaskazini mwa Iraq siku ya Alhamisi, kukitajwa kuwa kuhama kwa ghafla kunakowahusisha watu wengi. Jason Nyakundi na maelezo zaidi. (Taarifa ya Jason) Maafisa wa UNHCR walio nje wanasema kuwa watu wengi wanahama wakitumia daraja mpya [...]

16/08/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tiba endelevu ya afya ya akili kwa wahanga wa ghasia ni muhimu: WHO

Kusikiliza / Kambi ya wakimbizi Somalia

Katika kuelekea siku ya kimataifa ya usaidizi wa kibinadamu tarehe 19 mwezi huu, shirika la afya duniani WHO limetoa wito kwa tiba endelevu dhidi ya magonjwa ya akili kupatiwa kipaumbele hususan kwenye maeneo ya migogoro. Ripoti mpya ya WHO kuhusu huduma ya afya ya akili baada ya dharura, inasema mashirika ya misaada huwa yanahaha kutoa [...]

16/08/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tanzania kuadhimisha siku ya kimataifa ya vijana Jumamosi

Kusikiliza / Vijana wa Tanzania

Nchini Tanzania, Jumamosi ya tarehe 17 mwezi Agosti itakuwa ni kilele cha kitaifa cha siku ya vijana duniani ambapo maadhimisho hayo yatafanyika jijini Dar es salaam na hukoZanzibar. Taarifa ya Assumpta Massoi inafafanua zaidi. (Taarifa ya Assumpta) Ujumbe wa mwaka huu ni uhamiaji wa vijana na kusongesha mbele maendeleo ambapo Naibu Mkurugenzi kutoka Wizara ya [...]

16/08/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930