Nyumbani » 15/08/2013 Entries posted on “Agosti 15th, 2013”

Umoja wa Mataifa wazindua Mkakati wa kusaidia maendeleo Ramallah

Kusikiliza / un logo

Umoja wa Mataifa umezindua mkakati wa kusaidia maendeleo, UNDAF, kama sehemu ya kuleta pamoja juhudi za mashirika yote ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kuwasaidia watu wa Palestina, wakiwemo wakimbizi. Akiuzindua mkakati huo mjini Ramallah, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, amesema uzinduzi huo unaweka ukurasa mpya wa ushirikiano baina ya watu [...]

15/08/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama lataka machafuko yakomeshwe Misri

Kusikiliza / baraza la usalama

  Wanachama wa Baraza la Usalama wameelezea kusikitishwa na watu kufariki nchini Misri na kutaka machafuko yakomeshwe. Kwa mujibu wa taarifa ilosomwa na rais wa Baraza hilo kwa mwezi huu wa Agosti, Bi María Cristina Percevalwa Argentina, wanachama wa Baraza hilo wameelezea maombolezo yao kwa wahanga wa machafuko hayo. Kabla ya kufanya mazungumzo hayo ya [...]

15/08/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Washauri wa UM wahofia hali nchini Misri

Kusikiliza / egypt-clashes-12

Washauri wiwili maalum wa Umoja wa Mataifa wameelezea wasiwasi wao kuhusu machafuko yalotekelezwa Jumatano asubuhi nchini Misri, ambako vikosi vya usalama vimedaiwa kutumia nguvu zilokithiri dhidi ya waandamanaji mjini Cairo. Adama Dieng ambaye ni mshauri kuhusu kuzuia mauaji ya kimbari na Jennifer Welch, ambaye ni mshauri kuhusu wajibu wa kulinda, wamesema ingawa idadi kamili ya [...]

15/08/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama lapongeza kutekelezwa kwa mkataba kuhusu rasi ya Bakassi

Kusikiliza / Baraza la Usalama

Wanachama wa Baraza la Usalama leo wamekaribisha kuhitimishwa kwa kipindi maalum cha mpito mnamo Agosti 13 2013, ambacho kiliwekwa kuhusu rasi ya Bakassi, chini ya makubaliano ya Greentree. Baraza hilo la Usalama limezipongeza Cameroon na Nigeria kwa kutimiza ahadi zao na majukumu yao chini ya maamuzi yalofanywa na Mahakama ya Kimataifa ya Haki, na kwa [...]

15/08/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban akutana na viongozi wa Palestina huko Ramallah, alaani shambulio Lebanon

Kusikiliza / Katibu Mkuu ziarani Ramallah

Kuanza kwa mashauriano ya moja kwa moja kati ya Palestina na Israeli ni miongoni mwa ajenda za mazungumzo kati ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon na Rais wa Palestina Mahmoud Abbas mjini Ramallah. Bwana Ban amesifu uongozi wa Rais Abbas na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kwa kuwezesha kuanza tena kwa [...]

15/08/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WHO na UNICEF yaendesha kampeni ya chanjo dhidi ya polio, Mogadishu

Kusikiliza / Watoto wapokea chanjo ya polio

Shirika la Kuhudumia watoto katika Umoja wa Mataifa, UNICEF pamoja na Shirika la Afya duniani WHO linaendesha kampeni ya kutoa chanjo tangu kugunduliwa kwa visa vya  polio mjini Mogadishu nchini Somalia Ungana na Assumpta Massoi katika ripoti ifuatayo.

15/08/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Ban amteua Arancha Gonzalez wa Uhispania kama Mkuu wa ITC

Kusikiliza / Bi Arancha Gonzalez

  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, amemteua Arancha Gonzalez wa Uhispania kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Kimataifa cha Biashara, ITC, ambacho huwakilisha Kamati ya Biashara na Maendeleo katika Umoja wa Mataifa, UNCTAD na Shirika la Biashara Duniani, WTO katika  maendeleo ya kimataifa biashara. Bi Gonzalez atamrithi Patricia Francis wa Jamaica, ambaye [...]

15/08/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ban awapa heko watu wa Mali kwa uchaguzi wa urais

Kusikiliza / Ban awapongeza watu wa Mali kufuatia uchaguzi wa urais

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon, ametoa heko kwa mamlaka na watu waMalikwa kuendesha uchaguzi wa urais kwa njia ya ufanisi mnamo Julai 11, 2013. Wakati raia wa Mali wakisubiri kuthibitishwa kwa matokeo ya uchaguzi huo na Mahakama ya Kikatiba, Bwana Ban amempa hongera Bwana Ibrahim Boubacar Keїta kwa kuchaguliwa kuwa rais wa [...]

15/08/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Utafiti wa kiafya ndio njia ya pekee ya kuhakikisha kila moja amepata huduma:WHO

Kusikiliza / Kuna haja ya utafiti wa kiafya ili kuhakikisha upatikanaji wa huduma:WHO

Shirika la afya duniani WHO linazitaka nchi kuwekeza kwenye utafiti wa kimataifa wa kubuniwa kwa bima ya afya kwa kila mmoja na kwa kila nchi kote duniani. Jason Nyakundi na taarifa zaidi. (Taarifa ya Jason) WHO inasema kuwa kupitya kwa bima ya afya nchi zinaweza kuhakikisha kuwa wananchi wamapata huduma za afya wanazohitaji bila kuhangaishwa [...]

15/08/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Baraza Kuu lakutana kujadili Ushirikiano Mpya kwa Maendeleo ya Afrika, NEPAD

Kusikiliza / Baraza Kuu

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, leo limefanya kikao ambacho kimeangazia utekelezaji wa ushirikiano mpya wa maendeleo barani Afrika. Joshua Mmali ameufuatilia mkutano huo (TAARIFA YA JOSHUA MMALI) Katika kikao cha leo, wanachama wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa wamepitisha kwa kauli moja azimio kuhusu ushirikiano mpya wa maendeleo barani Afrika, NEPAD, na ambalo [...]

15/08/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Shehena ya misaada kwa wakimbizi wa Syria yaondoka Dubai: UNHCR

Kusikiliza / Shehena ya vifaa vya misaada kutoka UNHCR

Shehena kubwa zaidi ya misaada ya kibinadamu kwa ajili ya wakimbizi wa Syria kuwahi kusafirishwa na shirika la umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR kwa mwaka huu imeondoka Dubai, Falme za kiarabu Alhamisi. Shehena hiyo ikiwa na vifaa kama vile mablanketi kwa ajili ya watu Laki moja, vifaa vya jikoni zaidi ya seti Elfu [...]

15/08/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Wakulima wapata ugumu kuendesha mbinu zinazoendana vyema na tabianchi: FAO

Kusikiliza / Wakulima Tanzania

Matokeo ya awali ya mradi ulonuiwa kusaidia nchi za Malawi, Vietnam na Zambia kubadili mbinu za ukulima ili zikabiliane vyema na mabadiliko ya tabianchi, zinaonyesha kuwa baadhi ya wakulima wanapata ugumu kuendesha mbinu hizo mpya. Licha ya hayo, mradi huo pia umebainisha wakulima ambao wanabuni njia nzuri za kukabiliana na matatizo ya tabianchi kama vile [...]

15/08/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ban, Mfalme wa Jordan wafanya mazungumzo ya pamoja

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon na Mfalme Abdullah wa Jordan(picha ya faili)

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon leo amekutana na Mfalme Abdullah wa Jordan ambako wote wawili wamejadiliana juhudi zilizoanzishwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani John Kerry juu ya kurejesha upya mazungumzo ya upatanishi baina ya Israel na Palestina.   Ban alipongeza pia juhudi za Mfalme Abdullah pamoja na serikali yake [...]

15/08/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Pillay ataka hatua za dharura kuepusha janga zaidi nchini Misri

Kusikiliza / Navi Pillay

Kamishna Mkuu wa Haki za binadamu Navi Pillay amezisihi pande zote nchini Misri kujizuia kutumbukia kwenye janga zaidi baada ya siku moja ya umwagaji damu nchini humo Jumatano ambayo imesababisha vifo vya mamia ya watu na wengine kadhaa kujeruhiwa. Nalaani vikali vifo vya watu nchini Misri na nataka pande zote nchini humo kutafuta njia ya [...]

15/08/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Serikali ya Syria imeruhusu waangalizi wetu kuendesha mambo kwa uhuru-Ban

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametangaza kuwa serikali ya Syria hatimaye imekubali rasimi kutoa ushirikiano kuwezesha timu ya waangalizi kuendesha majukumu yake katika mazingira safi, salama na katika hali ya ufanisi. Amesema ujumbe wa Umoja wa Mataifa ulioko nchini humo sasa unaweza kuondoka katika muda wowote muafaka. George Njogopa na maelezo zaidi. (Taarifa ya [...]

15/08/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930