Nyumbani » 14/08/2013 Entries posted on “Agosti 14th, 2013”

Baraza la Usalama latiwa wasiwasi na hali ya usalama CAR

Kusikiliza / baraza la usalama

Wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, wameelezea wasiwasi wao kuhusu hali ya usalama katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, ambako utaratibu wa kisheria umesambaratika katika mazingira ya ukosefu wa uongozi wa kisheria. Mapema Jumatano asubuhi, Baraza hilo la Usalama limehutubiwa kuhusu hali nchini humo na Mwakilishi wa Katibu Mkuu na Mkuu wa [...]

14/08/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ukiukwaji wa haki za binadamu bado unaendelea CAR: Šimonović

Kusikiliza / Msaidizi wa Katibu Mkuu kuhusu Haki za Binadamu, Ivan Šimonović

Kati ya Disemba 2012 na Machi mwaka 2013, vikosi vya waasi wa Seleka na vikosi vya serikali ya zamani ya Jamhuri ya Afrika ya Kati vilitekeleza ukiukwaji mkubwa wa sheria za kimataifa za haki za binadamu na sheria za kibinadamu, ingawa uhalifu ulotekelezwa na waasi wa Seleka ulikuwa mwingi zaidi. Hayo yamesemwa na Msaidizi wa [...]

14/08/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

UNICEF imewekeza katika kutokomeza utapiamlo katika eneo la Mancha, Ethiopia

Kusikiliza / Watoto wa eneo la Mancha, Ethiopia

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF, kwa kushirikiana na serikali ya Ethiopia  na Muungano wa nchi za Ulaya linahaha kusaidia kutokomeza utapiamlo nchini humo.Mradi huu unanuia kutambua dalili za utapiamlo mapema na kuelimisha jamii kuhusu njia za kuuzuia.Ungana na Grace Kaneiya katika ripoti ifuatayo

14/08/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Mapigano ya kikabila huko Darfur Mashariki yanaathiri zaidi raia: Mkuu UNAMID

Kusikiliza / Ibn Chambas, UNAMID

Mwakilishi maalum wa ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika huko Darfur, UNAMID, Mohamed Ibn Chambas ameeleza wasiwasi wake vile ambavyo mapigano kati ya makabila ya Rezeiga na Ma'alia huko El Daein na Adila Darfur Mashariki yanavyozidi kuathiri raia. Amesema mapigano hayo yanapaswa kusitishwa mara moja kwa maslahi ya pande zote [...]

14/08/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama lajadili uimarishaji wa amani Afrika Magharibi na hali CAR

Kusikiliza / Babacar Gaye

  Hapa New York hii leo, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, limekutana kujadili suala la uimarishaji wa amani katika eneo la Afrika Magharibi, pamoja na hali katika Jamhuri ya Afrika ya Kati. Joshua Mmali ameufuatilia mkutano huo. (Taarifa ya Joshua) Mkutano wa leo wa Baraza la Usalama umeanza kwa wanachama kurithia taarifa ya [...]

14/08/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNESCO yalaani mauaji ya mwandishi nchini Guatamala.

Kusikiliza / Unesco yalaani mauaji

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO , Irina Bukova,  amelaani mauaji ya  mwandishi wa habari mkongwe wa radio huko nchini Guatamala anayeitwa  Luis de JesúsLima. Katika taarifa yake Bi Bukova ameitaka mamlaka nchini humo kufanya kila liwezekanalo kuwafikisha wahusika wa mauaji hayo katika vyombo vya sheria akisema [...]

14/08/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Wataalamu wa UM wawasili Nairobi kubaini athari za moto kwenye uwanja wa ndege

Kusikiliza / Uwanja wa JKIA ulipoteketea

  Jopo la wataalamu kutoka Umoja wa Mataifa limewasili nchini Kenya kufuatia ombi la serikali ya nchi hiyo kwa ajili ya kuchunguza athari za mazingira zinazoweza kuwa zimesababishwa na moto uliokumba eneo la wageni wanaowasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta wiki iliyopita. Jason Nyakundi na taarifa kamili TAARIFA YA JASON NYAKUNDI) [...]

14/08/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban ahitimisha ziara yake Pakistani aahidi ushirikiano

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-Moon na Waziri wa Pakistani Nawaz Sharif

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ambaye amehitimisha ziara yake nchini Pakistani tayari kuelekea Jordan amekuwa na mazungumzo na waziri Mkuu Nawaz Sharif ambapo wamejadili masuala kadhaa ikiwemo mchango wa Pakistani katika ulinzi wa amani, malengo ya maendeleo ya milenia na hali ilivyo nchini Afghanistan. Baada ya mazungumzo hayo, Bwana Ban na Bwana Sharif walishiriki [...]

14/08/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Naibu Katibu Mkuu asema ripoti ya huduma ya usafi na maji safi na salama kwa wote inatia moyo

Kusikiliza / Jan Eliasson, Naibu Katibu Mkuu wa UM

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Jan Eliasson amepongeza hatua zilizofikiwa katika kuhakikisha kila mkazi wa dunia anapata huduma ya majisafina salama bila kusahau matumizi ya vyoo kwa ajili ya kuweka mazingirasafi. Ametoa pongeza hizo kufuatia ripoti ya maendeleo ya kufanikisha hali hiyo iliyotolewa leo mjiniGeneva, Uswisi na jopo la ngazi ya juu lililoundwa [...]

14/08/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mfuko wa majanga ya dharura wa UM waidhinisha msaada wa fedha kwa Sudan Kusini

Kusikiliza / cerf logo

Mfuko wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kukabiliana na majanga ya dharura umeidhinisha dola Milioni Sita kwa ajili ya kusaidia mashirika ya misaada yanayosambaza huduma za chakula na mahitaji mengine nchini Sudan Kusini. Msaada huo ambayo pia inahusisha huduma ya majisafina salama unawalenga mamia ya wananchi walioathiriwa na machafuko katika eneo la Pibor kwenye [...]

14/08/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Katibu Mkuu alaani ghasia zilizosababisha vifo nchini Misri

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ambaye anahitimisha ziara yake Pakistani hii leo tayari kuelekea Jordan, amezungumzia ghasia zilizotokea mjini Cairo, Misri wakati vikosi vya usalama vikitawanya waandamanaji. Taarifa ya Joseph Msami inafafanua zaidi. (TAARIFA YA JOSEPH) Katika taarifa yake ya kulaani virugu hizo zilizotokea pale vikosi vya ulinzi vya Misri vilipotumia nguvu [...]

14/08/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Familia nyingi za wakimbizi nchini Tanzania zinakabiliwa na tatizo la kudumaa-WFP

Kusikiliza / wfp tanzania

Zaidi ya asilimia 35 ya familia za wakimbizi walioko katika kambi ya Nyarugusu Mkoani Kigoma wanakabiliwa na tatizo la kudumaa kunakosababishwa na ukosefu wa lishe bora, jambo ambalo linatishia usalama wa afya za wakimbizi wengi. George Njogopa na taarifa zaidi Pamoja na tatizo hilo, pia baadhi ya wakimbizi wanadaiwa kuishi katika hali ngumu na wakati [...]

14/08/2013 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Pillay aitaka Hamas kuacha kutekeleza hukumu ya kifo

Kusikiliza / Navi Pillay

Kamishna mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Navi Pillay  ameutaka utawala wa kundi la Hamas kwenye Ukanda wa Gaza kuachana na mipango ya kuwanyonga watu wanaokabiliwa na hukumu ya kifo kwa kuwa ni kinyume na sheria kimataifa kuhusu haki za binadamu.Mkuu wa sheria kwenye Ukanda wa Gaza alitoa matangazo kadha wakati wa [...]

14/08/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930