Nyumbani » 07/08/2013 Entries posted on “Agosti 7th, 2013”

Ban azungumza na Rais Kiir wa Sudan Kusini

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-Moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amekuwa na mazungumzo na Rais Salva Kiir waSudanKusini ambapo amemweleza kuwa amekuwa akifuatilia hali ilivyo nchini humo na kwamba hali ya utulivu imerejea baada ya mabadiliko ya baraza la mawaziri. Katika mazungumzo hayo kwa njia ya simu Bwana Ban pia amezungumzia azma ya Umoja wa Mataifa ya kuendelea [...]

07/08/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Kuachiwa kwa wafuasi wa Gbagbo ni hatua njema kuelekea maridhiano ya kitaifa Côte d'Ivoire

Kusikiliza / Doudou Diène

Mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya haki za binadamu nchini Côte d'Ivoire Doudou Diène amesema kitendo cha kuachiwa huru kwa wafuasi 14 wa Rais wa zamani wa nchi hiyo Laurent Gbagbo baada ya kuhusishwa na vurugu zilizotokea baada ya uchaguzi, ni hatua njema kuelekea maridhiano ya kitaifa.Wafuasi hao waliachiwa huru wiki hii [...]

07/08/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

"Hibakusha" akumbuka shambulio la Nagasaki mwaka 1945

Kusikiliza / Mji wa Nagasaki siku ya shambulio tarehe 09 Agosti 1945

Mwezi huu wa Agosti ni miaka Sitini na Minane tangu ndege za kimareknai zilipoangusha mabomu ya atomiki kwenye ardhi ya Japani hukoNagasakinaHiroshima. Maelfu waliuawa na maelfu walijeruhiwa huku idadi ya vifo ikiongezeka kila mwaka kutokana na madhara ya minunurisho ya nyuklia kwa manusura. Ripoti hii fupi ya Assumpta Massoi inakuletea kumbukumbu ya manusura au Hibakusha [...]

07/08/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Baraza Kuu lajadili mustakhbali wa vijana na maendeleo ya milenia

Kusikiliza / Mkutano wa vijana

Mkusanyiko wa kimataifa wa vijana umefanyika leo kwenye Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, ukiangazia kujenga uongozi wa vijana kwa ajili ya ufanisi wa malengo ya maendeleo ya milenia, MDGS. Joshua Mmali ana taarifa zaidi (TAARIFA YA JOSHUA) (WIMBO) Wimbo, wa kijana mmoja ambaye anashiriki mkusanyiko wa leo, wenye umbo la bunge la vijana. Kauli [...]

07/08/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Benki ya dunia yaidhinisha mradi wa umeme kwenye maporomoko ya mto Rusumo

Kusikiliza / Jim Yong Kim

Benki ya dunia kupitia bodi yake ya utendaji imeidhinisha dola Milioni 340 kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa uzalishaji wa umeme kwa kutumia nguvu za maji kwenye maporomoko ya mto Rusumo ulioko ukanda wa maziwa makuu barani Afrika.Mradi huo unalenga kunufaisha wakazi Milioni 62 walioko Burundi, Rwanda na Tanzania na unafuatia ziara ya Rais [...]

07/08/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mamia ya kina mama wajawazito wanahitaji msaada Syria:UNFPA

Kusikiliza / Mama na mwanawe(picha ya UNFPA)

Umoja wa Mataifa umesema kuwa umeanza kuingiwa na wasiwasi juu ya usalama wa raia Syria hasa wale walioko katika mji wa Homs ambako mapigano baina ya vikosi vya serikali na kundi la waasi yanaripotiwa kushika kasi.Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na idadi ya watu UNFPA limesema kuwa zaidi ya raia 400,000 wameendelea kusalia njia [...]

07/08/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Nchi zimetakiwa kuheshimu mikataba inayohusu watu wa asili:PIllay

Kusikiliza / Watu wa asili

Nchi zinapaswa kufanya juhudi zaidi za kuenzi na kuimarisha mikataba yao inayohusu watu wa asili, bila kujali ni lini ilitiwa saini. Hayo yamesemwa na kamishina mkuu wa haki za binadamu Navi Pillay katika taarifa yake ya maadhimisho ya siku ya kimataifa ya watu wa asili ambayo kila mwaka hufanyika Agost 9, George Njogopa na maelezo [...]

07/08/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WFP yatoa vocha za chakula kwa wakimbizi wa ndani Kordofan Kaskazini

Kusikiliza / WFP tyatoa vocha za chakula Kordofan

Wiki mbili baada ya watu wa Kordofan Kusini kukimbia machafuko kwenye vijiji vya Kordofan Kaskazini shirika la mpango wa chakula WFP limewapa vocha za chakula takribani wakimbizi wa ndani 33,000.WFP na jumuiya ya mwezi mwekundu ya Sudan wamegawa vocha hizo kwenye maeneo 35 katika vitongoji vitatu. Grace Kaneiya na maelezo zaidi. (TAARIFA YA GRACE KANEIYA) Kulipozuka [...]

07/08/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Watoto zaidi waachiliwa na jeshi la Myanmar:UNICEF

Kusikiliza / Watoto waliokuwa wameandikishwa jeshini

Mratibu wa Umoja wa mataifa nchini Myanmar na shirika la kuhudumia watoto UNICEF wamekaribisha hatua ya jeshi la Myanmar la kuwaachilia watoto na vijana 68 walikuwa jeshini. Jason Nyakundi na maelezo zaidi(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI) Hatua hii ya leo inajiri baada ya kuachiliwa kwa watoto wengine 42 na vijana wengine wa umri mdogo mwezi mmoja [...]

07/08/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Unyonyeshaji mtoto hupunguza uwezekano wa mama kupata saratani ya titi:UNICEF

Kusikiliza / Mtoto akinyonya

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF nchini Tanzania limetumia kilele cha wiki ya unyonyeshaji duniani kuelezea faida anazopata mama iwapo ataamua kuanza kumnyonyesha mtoto wake punde tu baada ya kujifungua. Mwakilishi wa UNICEF katika sherehe za kilele hicho zilizofanyika mjini Dar es salaam, Tanzania Dokta Jamal Malaga ametaja faida hizo kuwa ni [...]

07/08/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Walioathirika afya ya akili kutokana na kiwewe au kufiwa sasa kupata tiba: WHO

Kusikiliza / afya ya akili

Shirika la afya duniani WHO hii leo limetoa mwongozo mpya wa tiba dhidi ya watu waliokumbwa na athari ya afya ya akili kutokana na kiwewe au wanapopoteza wapendwa wao. "Tumechukua uamuzi huu baada ya kupokea maombi lukuki kutoka kwa watoa tiba ya maradhi ya akili kwa watu waliokumbwa na madhila hayo", ni kauli ya Dokta [...]

07/08/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031