WHO kutoa mwongozo kwa mahujaji kujilinda kutokana na homa ya Corona

Kusikiliza /

Shirika la Afya Duniani, WHO limesema licha ya baadhi ya watu kuhoji usalama wa mahujaji watakaokwenda Saudia kwa ajili ya Hajj, shirika hilo halina mipango yoyote ya kutoa ilani ya kubana usafiri kwenda huko kwa sababu ya virusi vya homa ya Corona, au MERS-CoV, ingawa kila hujaji anatakiwa kuchukuwa hatua za kujilinda binafsi na kuwalinda wenzie. Hata hivyo, WHO inapanga kutoa mapendekezo ya mwongozo ambao mahujaji watatakiwa kufuata katika siku chache zijazo.

Dk. Keiji Fufuda kutoka WHO amewaambia waandishi habari mjini Geneva kwamba, hadi sasa hakuna chanjo dhidi ya homa ya Corona, na kwamba watu wanapewa huduma za matibabu za ujumla tu, akiongeza kuwa ugonjwa huo unatia wasiwasi mkubwa, ingawa hauchukuliwi kama suala la afya la dharura kwa sasa.

Amesema ingawa imeamuliwa kuwa hali ya dharura kiafya isitangazwe kwa wakati huu, hali huenda ikabadilika katika siku zijazo. Amesema bado inahojiwa watu wanaambukizwa vipi virusi hivyo, na ni kwa nini, na kuongeza kuwa udhibiti wa maambukizi ni muhimu kwani mengi ya maambukizi yamefanyika katika vituo vya huduma za afya. Amesema WHO inashirikiana na nchi za Mashariki ya Kati na Uropa, na kutoa mapendekezo kuhusu jinsi ya kuimarisha uchunguzi.

 

 

 

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Mei 2017
T N T K J M P
« apr    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031