Wafanyakazi wa UM wamuenzi Mandela kwa kuwasaidia waathirika wa Sandy

Kusikiliza /

Wafanyi kazi wa UM

Katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya Mandela Umoja wa Mataifa unaungana na wito wa wakfu wa Mandela wa kutaka watu "kuchukua hatua na kuchagiza mabadiliko" wito ambao unawataka watu kujitolea kwa dakika 67 ili kuwasaidia wengine katika sehemu mbalimbali ikiwemo hospital, kufundisha watoto, kugawa chakula kwa wasio na makazi ,au shughuli yoyote ya huduma kwa jamii.

Kampeni ya dakika 67 inatokana na watu kujitolea kila dakika kwa kila mwaka ambao Mandela alijitolea kwa huduma za umma, kama wakili wa haki za binadamu, mfungwa, msaka amani wa kimataifa na rais wa kwanza aliyechaguliwa kidemokrasia baada ya ubaguzi wa rangi nchini Afrika ya Kusini.

Mwaka huu wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa kutoka vitengo mbalimbali walioko hapa New York wamemuenzi Mandela kwa kujitolea muda wao kusaidia kujenga nyumba zilizoharibiwa na kimbunga Sandy mwaka jana kwenye maeneo ya Long beach na Rockways.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930