UNHCR yatiwa wasiwasi na na hali tete inayoendela kushuhudiwa mashariki mwa DRC

Kusikiliza /

Idadi ya wakimbizi wanaoelekea Uganda inaongezeka:UNHCR

Baada ya majuma mawili ya mapigano kwenye mkoa wa kivu kaskazini , mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo hali ya raia katika eneo hilo inatia wasi wasi.Siku ya Jumapili sauti za mabomu na milio ya risasi vilikuwa vinasikika kwenye wilaya ya Bundibugyo iliyo magharibi mwa Uganda. Eneo hilo halifikiki kwa urahisi na mashirika ya kibinadamu na pia hali kwa wale ambao hawana uwezo wa kuingia nchini Uganda haijulikani .

Maelfu ya wakimbizi walianza kuingia mara ya kwanza nchini Uganda baada ya kutokea mapigano kati ya kundi la Allied Democratic Forces kutoka Uganda na jeshi la DRC mwezi huu. Kituo cha Bubukwanga kilicho umbali wa kimomita 25 kutoka kwenye mpaka sasa ni makao kwa wakimbizi 15,714 huku asilimia 60 kati yao wakiwa chini ya umri wa miaka 18.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031