UNESCO yapigia debe elimu kwa watoto wa kike

Kusikiliza /

Elimu ya mtoto wa kike yapigiwa debe

Katika kuadhimisha miaka kumi na sita ya mtoto mwanaharakati wa elimu Malala Yousfzai ambaye alijeruhiwa kwa risasi na watalibani huko Pakistani mwezi Oktoba mwaka jana kutokana na msimamo wake wa kutetea bayana elimu kwa mtoto wa kike shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi, na utamaduni UNESCO, limetaka kuwepo kwa fursa za elimu kwa mtoto wa kike hususani maeneo ambayo utamaduni hautoi mwana huo. Katika mahojiano na idhaa ya Kiswahili ya radio ya Umoja wa Mataifa  Afisa wa UNESCO jijini Dar es Salaam nchini Tanzania Elizabeth Kyondo amesema katika nchi zinazoendelea watoto wengi wa kike hunyimwa fursa sawa za kusoma tofauti na wale wa kiume jambo linalopaswa kutokomezwa hima kwa maendeleo ya jamii nzima

 (SAUTI YA ELIZABETH)

Bi Elizabeth amesema mbali na mila potofu pia umaskini, unachangia katika kumnyima mtoto wa kike fursa ya kusoma na hivyo kutaka nguvu ya pamoja ielekezwe katika kuhakiisha wasichana wanapata haki hiyo ya msingi.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Febuari 2016
T N T K J M P
« jan    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
29