Umoja wa Mataifa walaani shambulizi dhidi ya walinda amani nchini Sudan

Kusikiliza /

Baraza la Usalama lalaani mashambulizi dhidi ya walinda amani, Sudan

Wanachama wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa  wamelaani vikali shambulizi lililofanywa na watu wasiojulika dhidi ya kikosi cha pamoja cha Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika UNAMID,  kusini mwa jimbo la Darfur nchini Sudan mwishoni mwa juma wakati kikipiga doria.Kwenye shambulizi hilo walinda amani saba kutokaTanzaniawaliuawa  huku wengine 16 wakijeruhiwa. Wanachama hao walituma rambi rambi zao kwa familia za walinda usalama waliuouwa kwenye shambulizi na pia kwa serikali yaTanzaniana UNAMID.

Wanachama hao wameitaka serikali yaSudankufanya uchunguzi na kuwafikisha wahusika mbele ya sheria. Wote wamelitaja shambilizi hilo kuwa baya zaidi kuwahi kushuhudiwa tangu kutumwa kwa kikosi cha UNAMID nchini Sudan. Wamesema kuwa shambulizi lolote dhidi ya UNAMID halikubaliki na kutaka kutorudiwa tena kwa shambulizi kama hilo.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Aprili 2017
T N T K J M P
« mac    
 12
3456789
10111213141516
17181920212223
24252627282930