UM walaani umwagaji damu unaoendela Iraq

Kusikiliza /

Martin Kobler

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mtaifa nchini Iraq Martin Kobler amelaani shambulio lililogarimu maisha ya watu kadhaa jana nchini humo.

 

Amesema mashambulio hayo makubwa ya kigaidi kwa mara nyingine yalilenga raia wasio na hatia wanaofanya kazi zao za kila siku, kujenga mustakabali mwema kwao na watoto wao katika mazingira tete.

 

Mwakilishi huyo maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Matifa nchini Iraq amesema mashambulizi hayo yanakuja wiki mbili baada ya idadi kadhaa ya mashambulizi mengine yaliyoshuhudiwa yaliyolenga migahawa ,viwanja vya michezo , na sehemu nyinge zenye mikusanyikio inayosaidia kujenga mahusiano ambayo ni muhimu kwa mafanikio ya nchi.

 

Bwana Kobler pamoja na kutoa salamu za rambirambi kwa familia za wahanga na kuwatakiwa uponyaji wa haraka majeruhi pia ametaka mamlaka nchini humo kufanya kila linalowezekana kuwaokoa watu wa Iraq na umwagaji damu.

 

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2017
T N T K J M P
« jul    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031