Ujumbe wa UM ulioenda Syria wahimitisha ziara: Ban

Kusikiliza /

  

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon leo amekuwa na mazungumzo na Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani, John Kerry kwenye makao makuu ya umoja huo mjini New York, ambapo amesema timu aliyoituma Syria kufanya mazunguzo na serikali imehitimisha kazi yake leo na atapatiwa taarifa kuhusu ziara hiyo baadaye.

Bwana Ban amesema wakati umefika mzozo wa Syria upatiwe suluhu ya kisiasa kwani miaka Miwili na Nusu tangu kuanza kwa mzozo huo zaidi ya watu laki Moja wameuawa na mamilioni ni wakimbizi ndani ya nchi yao au nchi za kigeni.

(SAUTI YA BAN)

Ameunga mkono mazungumzo ya utatu kati ya Urusi, Marekani na Umoja wa Mataifa ambayo hufanyika Geneva na amesema atahakikisha yanafanyika haraka iwezekanavyo.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Julai 2017
T N T K J M P
« jun    
 12
3456789
10111213141516
17181920212223
24252627282930
31