Uchaguzi nchini Mali wasaidia kuunganisha wananchi: UNDP

Kusikiliza /

Maandalizi ya uchaguzi, Mali

Wakati kazi ya kuhesabu kura kufuatia uchaguzi wa Rais nchini Mali ikiwa inaendelea, Umoja wa Mataifa umesema uchaguzi huo wa kwanza kufanyika tangu mapigano makali kuzuka Kaskazini mwa nchi hiyo mwaka jana, umesaidia kuunganisha raia.Mwakilishi Mkazi wa shirika la mpango wa maendeleo la Umoja wa Mataifa, UNDP nchini Mali Aurelien Agbenonci amesema hayo katika mahojiano maalum na Radio ya Umoja wa Mataifa na kuongeza kuwa kupatikana kwa Rais kutachochea zaidi utekelezaji wa makubaliano ya Ouagadougou.

(SAUTI YA Agbenonci)

"Baada ya kile tunachofahamu kilitokea Kaskazini mwa nchi, ilikuwa ni vyema kuwa na mchakato huu wa uchaguzi ili kuunda serikali yenye mamlaka kamili, kuwa na utawala ambao utaleta pamoja jamii zote. Nafikiri kwamba serikali thabiti, Rais aliyechaguliwa kwa utaratibu atakuwa ni msingi kwa mchakato muhimu wa maridhiano."

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930