Serikali ziheshimu haki ya watu ya faragha: Mtaalam wa UM

Kusikiliza /

Frank La Rue

Uwezo wa serikali kufuatilia mienendo ya watu umewezesha kuingilia maisha ya watu binafsi, ambao huenda hata wasijue ikiwa wanatizamwa, au kuweza kupinga uvamizi kama huo dhidi ya maisha yao binafsi faraghani. Hayo yamesemwa na mtaalam maalum wa haki ya kujieleza katika Umoja wa Mataifa, Frank La Rue katika ripoti yake ya hivi karibuni zaidi, akisisitiza umuhimu wa serikali kuheshimu haki za faragha za watu binafsi na uhuru wa kujieleza, kama unavyobainika katika sheria ya kimataifa.

Mtaalam huyo amesema teknolojia ya kisasa imewezesha serikali kudhibiti mawasiliano ya mitandao, na hivyo kuwa na uwezo wa kusikiliza na kurekodi mawasiliano ya watu binafsi, kufuatilia simu za mkononi zilizotumika, kusoma ujumbe wanaotuma watu, na hata kufuatilia vinavyochapishwa kwenye tovuti, mitandao ya kijamii, blogu na aina zingine za mawasiliano.

Hata hivyo, amesema kama haki zingine, haki ya kuwa na faragha inaweza ikabanwa kwa kiasi fulani katika mazingira maalum, kama vile kukiwa na hofu kuhusu usalama wa kitaifa na vitendo vya uhalifu, ingawa sheria za kudhibiti umuhimu wa kubana haki hiyo, aghalabu hazitoshi katika mazingira ya kidemokrasia.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930