Ruhusuni raia na wafanyakazi wa misaada Homs na Aleppo: Pillay

Kusikiliza /

Kamishna Mkuu wa haki za binadamu, UM Navi Pillay

"Tuna wasiwasi mkuu kufuatia kuendela kwa ghasia katika maeneo ya Homs na Aleppo na athari za kibinadamu na haki za binadamu kwa watu wa kawaida''

Hiyo ni kauli ya Kamishna Mkuu wa haki za binadamu katika Umoja wa Mataifa Navi Pillay akizungumzia machafuko nchini Syria ambapo amesema watu kiasi cha 2,500 wako ndani ya Homs ambapo inaripotiwa bado makombora yanavurumishwa, silaha za masafa marefu na mashambulizi ya kutumia mizinga pia yanatajwa. Kadhalika uwepo wa kikundi cah upinzani chaenye silaha ndani ya makazi ya watu unaongeza hatari kwa raia.

Kamishna Pillay ameyataka makundi yanayokinzana kusimaisha mara moja vitendo vyote vinvyoweza kusababisha vifo vya raia, ili kuruhusu usalama kwa raia kuondoka Homs na pia kuruhusu misaada ya kibinadamu iwafikie. Licha ya mazungumzo kuendelea lakini si serikali wala vikundi vyenye silaha ambavyo vimetoa usalama wa kutosha kwa raia na wafanyakzi wa misaada.

Kadhalika pande hizo zimetakiwa kuheshimu wajibu wao katika haki za kimataifa za binadamu na haki za binadamu za kulinda raia na kuruhusu mashirika ya misaada yasiyo na upande wowote kuwafikia salama watu wenye mahitaji popote walipo nchini Syria.

Mashirika ya Umoja wa Mataifa na washirika wake yanasaidia watu ambao wameweza kuondoka Homs kwa usalama na wako katika miji na vijii jirani. Vyakula na mahitaji mengine ya lazima yameandaliwa ili kufikishwa Homs punde tu vikwazo vitakapoondolewa .

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031