Ripoti mpya ya ITU yaonyesha umuhimu wa mipango ya kitaifa ya vihamisha-data

Kusikiliza /

Mitambo ya mtandao

Nchi ambazo zimeweka mikakati ya kina ya kihamisha-data kasi, au broadband, zinafanya vyema zaidi kuliko zile ambazo hazijaitilia maanani njia hii ya mawasiliano.Hayo ni kwa mujibu wa ripoti mpya ilotolewa na Shirika la Kimataifa la Mawasiliano, ITU, Tume ya Kihamishadata kwa maendeleo ya dijitali na kampuni inayounda mitambo ya mitandao ya mawasiliano, Cisco.

Kulingana na utafiti mpya uliofanywa na watathmini wa ITU wa mipango kwa ajili ya maendeleo, takwimu zinaonyesha kuwa nchi ambazo zina mpango wa kitaifa wa kihamishadata zina utandawazi wa broadband wa asilimia 8.7 zaidi kuliko zile ambazo hazina.

Utafiti huo unaonyesha kuwa ukiacha mchango wa sababu kama vipato wastani vya juu, wingi wa masoko pamoja na kupanuka kwa miji, nchi zilizo na mipango ya broadband zinafaidika kwa asilimia 2.5 zaidi kuliko zile ambazo hazina, pengo ambalo linachukuliwa kuwa kubwa mno katika dunia ya sasa yenye uchumi wa utandawazi.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Julai 2016
T N T K J M P
« jun    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031