Raia walindwe, misaada iwafikie: UM

Kusikiliza /

Valerie Amos

Mkuu wa huduma za  misaada ya kibinadamu katika Umoja wa Mataifa, OCHA Valerie Amos ameelezea kusikitishwa kwake na kuzorota kwa huduma za utoaji misaada ya dhadura katika eneo la Pibor huko Jonglei nchini Sudan Kusini ambapo inakadiriwa watu laki moja wameshindwa kufikiwa ili kuokolewa kufuatia mapigano baina ya majeshi ya serikalia na vikosi vyenye  silaha na mapigano ya wanajamii.

Katika taarifa yake Bi Valerie Amos amesema mapigano yanatishia maisha ya raia na kupunguza uwezekano wa mashirika ya misaada kuwafikishia mahitaji, lakini akasifu kwamba kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa ghasia hizo, mashirika ya misaada yamefikisha misaada kwenye eneo liitwalo Dorein lililoko katika ziwa Kengen.

Hata hivyo, ameitaka jumuiya ya kimataifa kuhakikisha watoaji misaada wanapata vifaa muhimu  vya usafiri ikiwamo usafiri wa anga  ili kufikisha  mahitaji ya lazima mathalani chakula katika maeneo yasofikiwa kwa urahisi kwa usafiri wa barabarani.

Bi Amos amezitaka pande zinazopigana kusitisha mapigano hima ili kunusuru vifo vinavyoweza kuepukika, na kuzuia misaada kuwafikia wahitaji, huku pia akitaka kuheshimiwa kwa sheria za kimataifa za kibinadamu zinazotaka ulinzi dhidi ya raia.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031