Namibia na Angola zakabiliwa na ukame :UNICEF

Kusikiliza /

Namibia na Angola zakabiliwa na ukame

Namibia na Angola zinakabiliwa na ukame unaotishia usalama wa chakula  na kuathiri watoto katika pande zote za mipaka ya nchi hizo. Japo dharura hii iko katika hatua za mwanzo lakini hali inatarajiwa kuzorota.Grace Kaneiya anafanunua zaidi.(TAARIFA YA GRACE)

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na watoto UNICEF linasaka uungwaji mkono toka Jumuiya ya Kimataifa kwa ajili ya kutoa msaada katika maeneo ya watu walioathirika.

Shabaha ya UNICEF ni kuwapiga jeki wanawake na watoto ambao wanaandamwa na matatizo ya ukosefu wa lishe bora na matatizo ya kiafya katika nchi zote zilizokumbwa na ukame.

Uungwaji mkono wa UNICEF kwa nchi zaAngolanaNamibiaumelenga zaidi kukinga na kutoa matibabu katika maeneo ya ukosefu wa lishe bora na lile linalohusu afya.Patrick McCormick ni afisa wa UNICEF

(SAUTI YA PATRICK McCORMICK)

 UNICEF nchiniNamibiainahitaji kiasi cha dola milioni 7.4 million wakati nchiniAngola UNICEF inahitaji dola milioni 14.3.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2017
T N T K J M P
« jul    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031