Muafaka wa Australia-Papua New Guinea kwa waoomba hifadhi ni changamoto:UNHCR

Kusikiliza /

Waomba hifadhi huwasili kwa boti

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limetathimini hatua zilizotangazwa na serikali ya Australia mwezi huu kuhusu kuwasili kwa boti waomba hifadhi nchini humo.UNHCR inasema inatambu kuwa hatua hizi zinachukuliwa dhidi ya ongezeko la watu wanaowasili kwa watu ambao wanadhulumiwa na wanatumia njia hatari ya bahari wakiwemo familia, watoto wasio na waangalizi na watu wengine wasiojiweza.

Lakini pia imesema inaafiki hofu ya serikali yaAustralia kuhusu hatari ya watu kupoteza aisha inayoambatana na safari hizo, na imeahidi kushughulikia changamoto zinazosababishwa na waoomba hifadhi hao kuwasili kwa njia ya boti, kwaAustralia na nchi zingine.

UNHCR imeishukuru timu ya uokozi yaAustralia na Indonesia,kwani kwa msaada wao maisha ya watu wengi yameokolewa. Pia imesema Australia inastahili kutambuliwa kama moja ya nchi wasamaria kwa kutoa makazi kwa waomba hifadhi.

UNHCR inasema hatua mpya zilizochukuliwa hazina viwango vinavyostahili vya kuwalinda waomba hifadhi na wakimbizi  Papa New Guinea na kuacha maswali mengi ya serikali ya Papua New Guinea bila majibu.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Febuari 2016
T N T K J M P
« jan    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
29