Mpango wa kuikwamua Somalia kutoka kwenye hali ya sasa wazinduliwa

Kusikiliza /

Hassan Sheikh Mohamoud

Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamoud amesema kuwa nchi yake imekaribisha mpango mpya kutoka kwa mataifa yaliyoathiriwa zaidi ya mizozo ya g7+ wa kuikwamua nchi hiyo kutoka kwenye hali iliyopo sasa. Rais Hassan Sheikh Mohamoud ameyasema haya  alipokwa akitoa hotuba kwenye mkutano kuhusu mipango ya kisiasa ya hadi mwaka 2016 mjini Mogadishu.Mkutano huo uliwashirikisha maafisa wa ngazi za juu kwenye serikali ya Somalia, wakilishi wa mashirika ya umma na wanachama kutoka jamii ya kimataifa ambapo walizungumzia mipango ambayo itaorodhesha malengo ya serikali kabla ya mkutano ambao utaandaliwa Septemba 16 mjini Brussels.

Mkurugenzi kwenye muungano wa Ulaya kanda ya Afrika Nick Westcott amekaribisha kujumuishwa kwa serikali ya Somalia akiongeza kuwa Muungano wa Ulaya utatuma wajumbe nchini Somalia na eneo la Puntland kuhakikisha kuwa wasomali wote wameshiriki kwenye mpango huu.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Mei 2017
T N T K J M P
« apr    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031